HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2017

KInana Kuzindua Kampeni za CCM Jimbo la Dimani leo, CUF Kuzindua Jumapili

Na Talib Ussi, Zanzibar

Vyama vya CCM na CUF ambavyo vina upinzani mkubwa katika changuzi mbalimbali visiwani Zanzibar vitazindua kampeni zao katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani  ambapo makatibu wakuu wa vyama hivyo watakuwa wageni rasmi.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kitazindua kampeni zake hizo katika mbio za kumpata mrithi wa hafidhi Ali Tahir  leo ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ndie mkuu wa shuhuli hiyo.


Hayo yalithibitishwa na  katibu wa idara ya kamati maalum idara ya itikadi na uwenezi  Zanzibar Warride Bakari Jabu alisema kuwa kampeni hizo ambazi zitafanyika katika kiwanja cha Maungani zitazinduliwa na katibu mkuu wa CCM zitaaza kwa shamra shamra za aina yake.


“Tumepanga safu imara ambayo tunaimani ya kulirudisha jimbo letu ambayo itaongozwa na katibu mkuu huyo na naibu wake kwa upande wa Zanzibar Vuai Ali Vuai na katibu mwenezi na Itikadi Hafrei Polepole” alieelza Waride.

Wakati hayo yakiwa kwa upande wa CCm ama kwa watani wao wa jadi chama Cha Wananchi CUF kitarajiwa kufanya uzinduzi wao siku ya Jumapili ambapo Katika Mkuu wao Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakayefan ya uzinduzi huo katika vita vya kuwania kiti hicho.

Mkurugenzi wa Chaguzi na Bunge CUF, Omar Ali Shehe alisema kwa kushirikiana na wanachama wao kuhakikisha kuwa wanarithi kiti hicho.

Sambamba na hilo alisema Chama hicho kinawawakilisha Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) na viongozi mbali kutoka umaoja huo watashiriki katika kampeni hizo kuhakikisha wanashinda.

“Hatuna wasi wowote tunakwenda kulichukua jimbo kwa njia ya kidemokrasi kama wao wamezea ubabe na wafanye lakini sisi wapiga kura wetu ndio silaha yetu” alieleza Shehe.

Jimbo la Dimani limekuwa wazi kutoka na alikyekuwa Mbunge wa Jimbon hilo kufariki mwezi ulioipita Hafidhi tahiri ambapo vyama kumi na moja vimejitokeza katika kuwania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages