HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 21, 2017

CUF WAHITIMISHA KAMPENI JIMBO LA DIMANI

 Katiu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa kufunga kampeni katika jimbo la Dimani mjini Zanzibar.
 Kikundi cha Brassband ya Chama cha wananchi CUF, ikitumbuiza kwenye mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF), kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Mbunge wa Dimani Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wa chama hicho na viongozi wa Chadema kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Mbunge wa Dimani Zanzibar.

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wakati  wananchi wa Jimbo la dimani wakijiandaa kupiga kura leo katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge, magari ya kivita aina Deraya na Vikosi mbali mbali vya ulinzi vimekuwa vikiranda katika maneo mbali katika kisiwa cha Unguja huku wengine wakijifunika nyusoo.

Magari hayo ambayo yalikua yamejaa majeshi na Polisi na vile vikosi vya  Zanzibar vilianza jana katika viwan ja tofauti na huku wakiwa wamevalia mavazi kamili ya kivita.

Makamu wa kwanza mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka wananchi walihudhuria kwa wingi na wahudhurie wa wingi katika vituo vya kupiga kura.

Alieleza kuwa uchaguzi huo ni uchaguzi wa aina yake kwani kama wananchi watachagua mabadiliko basi wataionesha CCM kuwa hawana tena nafasi katika majimbo ya Zanzibar.
“Mkimchagua Abdul-razak itakua sawa na kuonesha Dunia kuwa sisi CCM hatuitaki tenaaaa” alieleza Maalim Seif.

Alisema kuwa tangu walipojiwekaa madarakani hawana mabadiliko yoyote waliyoyafanya na kudai hata wakikaa miaka mia hawana uwezo wa kuleta mabadiliko.

“Wallah hawa hata wakaee miaka mia hawana uwezo wa kuleta mabadiliko, labda kuwaadhibu wananchi wao, ninachokuombeni tumchague Abdul-razak ili tulete mabadiliko” alieleza Maalim Seif.

Alieleza kuw an nia yake ya kuifanyia mabadiliko makubwa Zanzibar kama ilivyo Singapoor iko pale pale, kwani wananchi wengi maisha yao yamekuwa magumu.

“Hawa walitangaza Elimu Bure lakini leo wanachangisha wananchi vikalio vya shule ndio bure hiyoo” aliuliza Maalim Seif.

Alieleza kuwa sasa Dk. Shein hana uwezo wa kuleta mabadiliko yoyote na badala yake sasa atumie vikosi vya SMZ kuwatisha wananchi.

Sambamba na hilo kuhusu kero za Muungano Maalim Seif alieeza kuwa viongozi wa CCM hukaa kwenye vikao vyao na kudai keron hizo zimekwisha na kueleza kuwa hakuna kero hata moja walioitatua.

Leo wananchi wa Zanzibar wakipeleka bidhaa zao Tanzania bara wanatolewa kodi hata kama Zanzibar tayari wametozwa kodi hiyo.

Kuhusu suala la mabalozi Maalim Seif alieleza kuwa Balozi zoote ambazo wanapelekwa Wazanzibar ni zile tuu nchi ambazo zinawatu wengi wenye asili ya Zanzibar kama nchi za kiarabu, ambazo alidai sauti yake ni ndogo.

“Leo hii ni siku yenu watu wa Dimani kufanya maamuzi makubwa ya kuiangusha CCM katika nafasi hii ya Ubunge” alieleza maalim.

Ama kuhusu kuhusu Uchaguzi uliofutwa aliwataka wanachama wa CUF kutembea kifua mbele kwa wao walishidanda katumeshintika uchaguzi huo.

"haki yetu ipoo wacheni wasiwasi sisi tumeshindaa ondoeni ghofu" alieleza maalim Seif.

Jana ikiwa siku ya kuchukua vitambulisho vya mawakala, katika vituo vya Tume ya Uchaguzi Taifa NEC vilikua vimezungukwa na Jeshi la Polisi kitu ambacho walipofika mawakala wa Chama cha wananchi CUF na kufukuzwa kama vile hawajuilikani.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mkurugenzi wa Uchaguzi na MIpango wa Chama hicho Omar Ali Shehe alieleza kuwa mawakala wake wamefukuzwa kama magaidi wakati waliitwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo kwa ajili kuchukua vitambulisho vyao hivyo.

Sambamba na hilo Shehe aliwataka wanachama wa CUF kuwa makaini katika kulinda kura na kuwazuia wote wale Mamluki walipangwa kupiga kura Jimboni humo.

Alidai kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeshaweka watu kutoka maeneo tofauti nili waje wapige kura leo jambo aliwataka  wananchi hao wawe tayari na maluki hao.

“Kama wametaka Fujo sawa waache walete hao watu wao, tutambana  nao vyovyote vile wanavyotaka, tukotayari, kwani NEC tumeshawaeleza na hawako tayari kuchukua hatua” alieeza Shehe.

Aliwataka wapiga kura wa Dimani kumpigia kura Mgombea wa Chama chao ambaye anawakilisha vyama vilivyoundaa umoja wa Ukawa Adbul-Razaki Khatib Ramadhan kwa kura nyingi ili aweze kuwa mbunge wao kwa maslahi ya nchi yao.

“Kama bado tunataka tugomboke na dhulma hizi za CCM basi nakuombeni kwa heshima zoote tumchagueni mbunge kutoka CUF” alielza Shehe.

Akizungumza katika mkutano huo Nasour Ahmed Mazurui alisema licha ya vitisho wanavyovitoa Jeshi la Polisi na vikosi washirika, wataenedelea kupiga kura kwa ajili ya kuing’oa CCM katika Jimbo hilo.

“Nikawaida yao kututisha sisi hawa, msiwaogopee sisi kazi yetu moja tufike mapema kwenye vituo ili kumueka mbunge wetu madarakani” alieleza Mazurui.

Mkutano huo ulihudhuriwaa na viongozi mbali mbali wanaounda UKAWA akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalim na viongozi wengine wa NCCR-Mageuzi  na NLD.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalim aliwataka Wananchi wasifanye kosa leo katika kisanduku cha Uchaguzi ili kuhakikisha Mgombea wa CUF anashinda katika uchaguzi huu wa Leo.

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wanakimbilia Upinzani kwa sababu ndio ambapo wanaelezwa maneno ya haki ambayo yanwapa matumaini ya Maisha yao.

“Ndugu zangu tuwezoeni hawa, hata walete ndege za kivita hatutokipigia kura CCM abadani” alieleza Mwalim.

Wakati akizungumza katika Jukwaa Mwalima Magari ya Vokosi vya SMZ wale ambao wamejificha Nyuso walipita katika bara bara  kama magari manne yakiwa yameongozanaa.

“Wananchi maisha yamekuwa magumu sanaa kwa sababu ya dhulma zinazofanywa na CCM dhidi ya wananchi waliowengi” alieleza Mwalim.

Alisema yeye binafsi kaingia katika Upinzani na kuiacha CCM kwa lengo la kupigania haki ya wanyonge ambayo CCM imeshindwa kufikia.

Aliwata wnanchi wa Dimani waiende kupiga Kura kwa ushabiki, bali wapige kura kwa CUF ili wapate matumaini mapya katika Jimbo hilo.

“Maisha yetu jamani hatuyaamui kwa kadi za vyama bali ni kura twendeni tukamchague Abdul-razak ili asimamie shida zetu” alieleza Mwalim.

Alieleza kuwa kwa kipindi kirefu CCM wameshamalizika na kudai sasa Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ ndio wanaopigia kura CCM.

“CCM tumewashinda Pande zote mbili lakini Jeshi ndilo ambalo lilizunguka eneo la Bwawani ili wapore ushindi wa Ukawa” alieleza Mwalimu.

“Hawa wamezoe kuiba kura tuu, na hawan tena mapenzi kwa wananchi ndio ukoana kila pembe wanawapiga wannachi kwa kutumia kikosi cha Mazombi” aliendelea.

Aliwata IGP wa Jeshi la Polisi Tanzania  na Waziri wa Mambo ya Ndani kuhakikisha usalama wa wapiga kura wa Dimani kwa kile alichodai vitisho vimekuwa vikubwa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment

Pages