HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 08, 2017

CUF YAZINDUA RASMI KAMPENI ZAKE JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika Jimbo la Dimani uliofanyika Fuoni Uwanja wa Mpira mjini Zanzibar. (Picha zote na Talib Ussi).
 Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akimnadi mgombea wa chama hicho katika Jimbo la Dimani, Abdulrazaki Khatib Ramadhani wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Dimani uliofanyika Uwanja wa Mpira Fuoni mjini Zanzibar.
Kumnadi mgombea.
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika Fuoni Uwanja wa Mpira mjini Zanzibar.
Waziri Mkuu za zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akipeana mkono na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad baada ya katika mkutano wa uzinduzi kampeni uliofanyika leo Fuoni Uwanja wa Mpira mjini Zanzibar. 
Aliyekuwa mgombea Urais katika uchaguzi wa 2015 kupitia Chadema kupitia UKAWA, Edward Lowassa akisalimiana na aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema kupitia UKAWA, Juma Haji Duni wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani.
 Wanachama na wafuasi wa CUF waliojitokeza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni.
 Kampeni Zanzibar.
 Wanachama na wafuasi wa CUF mkutanoni.
Na Talib Ussi, Zanzibar

Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), umesema Serikali iliyopo madarakani licha ya kujigamba imechaguliwa na wananchi lakini imekuwa na vitisho vikubwa kwa wananchi wake hasa wa kipato cha chini.

Kauli hiyo ilitolewa na aliyekuwa  mgombea wa Urasi wa vyama vinavyounda umoja huo, Edwar Lowassa  mara baada ya uchaguzi wamekuwa wakiwatisha wananchi kwa kuwavunjia majumba yao na kuzuia mikutano hadhara.

Alieleza kuwa hiyo ni dalili kuwa utawala uliopo umejiweka kwa nguvu na hauna ridhaa ya wannachi na kuwataka wananchi wasitishike mabadiliko ni lazima bara na Zanzibar.
“Mabadiliko  Tanzania hayawezi kuzuilika hivyo aliwataka wananchama wa vyama vya upinzani kutokata tama” alieleza Lowassa.

Lowassa alieleza kuwa anaamini uchaguzi uliopita alishinda lakini kwa kuhofia kuingiza nchi kwenye matatizo aliamua kukaa kimya licha ya makundi makubwa ya vijana kumtaka awaruhusu kudai haki yao.

Sambamba na hilo alielezakuwa  hali ya kisiasa iliopo sasa Tanzania ni nchi inaongozwa kibabe bila ya kutumia democrasia huku ikikumbwa na janga kubwa la njaa.
‘’Ni wahakikishie wananchi wa Zanzibar na watanzania wote ni kwamba vyama vya upinzani vilishinda bali waliiba kura’’alifafanua zaid Lowasa.

Alitoa wito kwa wananchi wote kutanua fikra zao kwa sasa serikali inaelekea kubaya zaidi na ni wakati  kwa watanzania kuendelea kufanya maamuzi makubwa zaidi katika uchaguzi unaokuja 2020 kwa upande wa Tanzania.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF ), Maalim Seif Sharif Hamad alisema umoja wa vyama vya ukawa utaendelea kushikamana maana umeleta tija kubwa kwa wananchi.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wananachi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka wananchi kutembea kifua mbele na huku wakijua wao nin washindi wa uchaguzi uliopita na kudai hila za CCM zimegonga mwamba.

“Sisi ni washindi hata wakiwatisha msigope, tutapambana hadi mwisho lakini haki yetu lazime kwa uwezo wa allah irudi kwani ni maamuzin yetu” alieleza Maalim Seif.

Waacheni wajidanganye, na huku wakiendelea kuwatisha wananachi lakini tusema mwaka huu hawana salama na tutawaondoa kwa nguvu za Mungu.

Kwa upande mwengine maalim Seif alieleza kuwa Serikali aliyadai kuwa ni ya  dhulma imeweza kuwavunjia wananchi wao maeneo yao ambayo wanapata riski zao na kudai ni msaada kwa serikali hiyo katiika kupunguza uzito wa Ajira.

“Huyo anayejiita Rais  anajigamba eti anakusanya kodi, lakini anawavunjia wananchi wake maduka yao bila kujali hali zao” alieleza Maalim Seif.

“Umasikini umezidi kutokana na utawala mbovu, kila siku wanawapiga wananchi mabomu bila ya sababu eti kwa sababu tuu eti rais wao hatajwi kwenye Hutba za miskiti” alielendelea.

Alieleza kuwa licha ya umasikini huo Serikali hiyo aliyodai kuwa sio halali imefika hatua ya kuwanyanganya wananchi Mifugo yao bila kujali hali zao za maisha.

Viongozi wa CCM kutoka Bara wamezoea kuja Zanzibar kutia Fitna tuu kwa wazanzibar.

Aliwataka wazanzibar kuwapuuza na kuwaomba wananchi wasichokozeke kwani juhudi za kudai kile walichokiita haki yao zimeshafikia hatua nzuri.

“Subra yenu ndio Nguvu yangu katika kudai haki yenu bila papara na in Sha Allah tuko karibu kupata tulichoporwa” alieleza Maalim Seif.

No comments:

Post a Comment

Pages