HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 18, 2017

HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA NCHINI NI YA KURIDHISHA

 Mwenyekiti wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, Bw.  Mohamed Salum akielezea jambo kwa mwandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula katika Soko hilo leo jijini Dar es Salaam. Mohamed amesema kuwa chakula kinapatikana kwa wingi kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa.
Picha ikionyesha baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam. 
KS3: Mkazi wa jijini Dar es Salaam akinunua nafaka katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

Na Frank Shija – MAELEZO

HALI ya upatikanaji wa chakula nchini inaridhisha licha ya changamoto ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa za chakula zitokanazo na nafaka.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, Bwana Mohamed Salum katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Mohamed amesema kuwa pamoja na kuwa Dar es Salaam inategemea chakula kutoka mikoani bado hali ya upatikanaji wake ni mkubwa na wa kuridhisha kama ambavyo imekuwa miaka ya nyuma.
“Chakula bado kinapatika kwa wingi japo changamoto iliyopo ni ongezeko la bei pekee kitu ambacho si kigeni duniani kote,” alisema Salum.
Alisema nia ajabu sana kusikia watu wanasema kuna baa la njaa wakati vyakula vinapatikana kwa wingi katika masoko yetu.
Aliongeza kuwa kungekuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi hata uingizwaji wa chakula katika jiji la Dar es Salaam ungepungua kwani asilimia kubwa inategemea chakula kutoka mikoani, badala yake upatikanaji wa chakula umeendelea kuwa wa kuridhisha.
“Ndugu mwandishi ukitaka kujua kuwa hakuna uhaba wa chakula jaribu kutembelea maeneo ya Manzese Uzuri utajionea namna maroli matani kwa matani yanayoingiza nafaka kwenye mashine za kusaga na kukoboa.” Alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Pages