Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

.

CRDB

CRDB
.

Pages

MAELEZO YABAINI NYARAKA FEKI ZA KUSAJILIA GAZETI

MkurugenziIdarayaHabari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari hawapo (hawapo Pichani) kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya FAKUNA ambaye anatuhumiwa kutaka kuitapeli Serikali baada ya kubainika kuwasilisha nyaraka za kughushi ili asajili Gazeti la Lete Mambo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Msajili wa Magazeti, Patrick Kipangula na kushoto ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Lilian Lundo.
 Mtuhumiwa wa kughushi nyaraka za Serikali ili asajili Gazeti ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya FAKUNA, Joseph Sheka akitolewa ndani ya Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dk. Hassan Abbasi  kumkabidhi mtuhumiwa huyo mikononi mwa jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi. (Pichana na Frank Shija – MAELEZO).
Mtuhumiwa, Joseph Sheka akiongozwa na Askari Kanzu kuelekea kwenye gari la Polisi tayari kwa kupelekwa Kituo cha Polisi Kati leo jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa wakiwa ndani ya Gari la Polisi mara baada ya kukamatwa na kukabidhiwa kwa jeshi la Polisi.

Na Jacquiline Mrisho

Idara ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili gazeti la LETE MAMBO.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka mbalimbali akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa awali umebaini kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo zilizotumiwa ni za kughushi.

“Ni vyema jamii ikafahamu kuwa huu sio wakati wa kujaribu kuishi kwa njia zisizo halali, kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika pindi anapotaka kupatiwa huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Umma.

Dkt. Abbasi alitoa rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka zinazowasilishwa na wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kuiingiza Serikali katika matatizo hivyo kuitia hasara.

Mbali na hayo Dkt abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake.

Kwa sasa Idara ya Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini dar es salaam kwa mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment