HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 24, 2017

MAENDELEO BANK WASOGEZA FURSA KWA WAFANYABIASHARA KARIAKOO

  Askofu Mkuu wa Diosisi ya Mashariki na Pwani wa kanisa la KKKT Dkt Alex Malasusa Amewaasa wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kujifunza njia sahihi ya kuhifadhi akiba kwenye mabenki ili kuepukana matatizo yanayoweza kuwakumba kama kuibiwa fedha hususani katika kipindi hiki kigumu cha upatikanaji wa fedha. Pia aliwaomba kuitumia Maendeleo Bank kwa ajili ya biashara zao kupitia huduma za mikopo.
 Askofu Malasusa ameyasema hayo tarehe 23.01.2017 alipokuwa akizungumza na Fahari news katika uzinduzi wa tawi jipya la benki ya (Maendeleo Bank) lililozinduliwa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa tawi hilo jipya Bi Nuru Shedrack alisema uzinduzi wa tawi hilo la Kariakoo linatoa fursa kwa wafanyabiashara kwa kusogezewa huduma ya kibenki karibu na sehemu zao za kazi ili kuepuka usumbufu na hatari ya kutembea na fedha jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao.
Aidha Bi Nuru alifafanua kuwa licha ya Maendeleo Bank kuwa chini ya Kanisa la KKKT ila Benki hiyo inalenga kutoa huduma kwa watu wote bila kujali itikadi za Kidini, Chama wala Kabila.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba alisema Bank ya Maendeleo itaendelea kuboresha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na Kusogeza Karibu zaidi Huduma zake kwa wateja.
Hili ni tawi la tatu kuzinduliwa na Benki hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo tawi la kwanza lilizinduliwa Novemba mwaka 2016 eneo la Mwenge Jijini hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages