HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 10, 2017

MBUNGE WA TANGA AWAPA POLE WATU WALIOPOTEZA NDUGU ZAO AJALI YA KUZAMA KWA JAHAZI

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi  kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika kipindi hiki kigumu.

Ajali ya Jahazi  ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria  12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.

Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi  na kuzama.

Akizungumza na MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.

Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.

Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

 “Ajali sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.

Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.

Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.

Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.

Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu mengine.

No comments:

Post a Comment

Pages