HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2017

BEI YA UMEME YAONDOKA NA MKURUGENZI TANESCO


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakati waziri Muhongo alipotembelea Makao Makuu ya TANESCO Desemba 12. 2015. Rais Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi huyo. (Picha ya Maktaba).

Na Mwandishi Wetu

SAKATA la kupanda kwa bei mpya ya umeme limechukua sura mpya, baada ya Rais John Magufuli kumtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kutumbuliwa kwa Mramba, ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kuzuia utekelezaji wa bei mpya ya umeme zilizopangwa kuanza kutumika Januari 2.

Desemba 30, mwaKa jana Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi alitangaza bei ya umeme kupanda kwa asilimia 8.5.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa Rais Dk. John Magufuli leo Januari 1, 2017 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Mramba.


Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Dk. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco ambapo uteuzi huo Dk. Mwinuka unaanza mara moja.

No comments:

Post a Comment

Pages