HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 06, 2017

Onyango alivyovaa viatu vya Samatta Tuzo za CAF 2016










ABUJA, NIGERIA

HATIMAYE kitedawili cha Tuzo Ubora za Shirikisho la Soka Afrika (The 2016 GLO-CAF Awards), kimeteguliwa usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa International Conference Centre, jijini Abuja, Nigeria kwa washindi kujulikana.

Kupitia hafla hiyo, mlinda mlango wa kimataifa wa Uganda, Dennis Onyango anayeidakia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, aliibuka Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza ligi ya ndani, akivhukua mikoba ya Mtanzania Mbwana Samatta aliyetwaa mwaka jana. 

Nyota wa kimataifa wa Algeria anayekipiga Leicester City, mshambuliaji Riyad Mahrez aliibuka na tzuo kubwa zaidi ya zote ya Mchezaji Bora wa Afrika, alikowafunika Pierre Emerick Aubameyang wa Gabon na Msenegal, Sadio Mane walioshika nafasi ya pili na tatu.

Ulikuwa usiku wa aina yake pia kwa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ambaye alitangazwa mshindi wa Tuzo ya CAF Platinum, huku Wanigeria Kelechi Iheanacho, Alex Iwobi na Asisat Oshoala wakiibuka na tuzo mbalimbali katika usiku huko.

Washindi wa Tuzo za GLO-CAF 2016

1. Timu Bora ya Mwaka (National Team of the Year): Uganda ‘The Cranes’

2. Timu Bora ya Taifa ya Mwaka kwa Soka la Wanawake (Women’s National Team of the Year): Super Falcons ya Nigeria 

3. Klabu Bora ya Mwaka (African Club of the Year): Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini

4. Tuzo ya Kipaji Bora Kinachochipukia (Most Promising Talent): Kelechi Ihenacho, Mnigeria anayechezea Manchester City

5. Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka (Youth Player of the Year): Alex Iwobi wa Nigeria anayekipiga katika klabu ya Arsenal

6. Kocha Bora wa Mwaka (Coach of the Year): Pitso Mosimane wa klabu ya Mamelodi Sundowns, aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika

7. Mchezaji Bora wa Mwaka wa Soka la Wanawake (Women’s Player of the Year): Asisat Oshoala wa timu ya taifa ya Nigeria, anayechezea klabu ya wanawake ya Arsenal

8. Mwamuzi Bora wa Mwaka (Referee of the Year): Bakary Papa Gassama wa Gambia

9. Tuzo ya Nguli Bora (Legend Award): Laurent Pokou, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na Emilienne Mbango, nyota wa zamani wa Cameroon

10. Mchezaji Bora wa Afrika - Anayecheza Ligi za Ndani (African Based Player of the Year Mshindi): 
Mshindi wa Kwanza: Denis Onyango, kipa wa Uganda na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
Mshindi wa Pili: Khama Billiat wa Zimbabwe na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
Mshindi wa Tatu: Rainford Kalaba, Mzambia anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

11. Kikosi Bora cha Mwaka (Team of the Year): Kipa: Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns)
Mabeki: Serge Aurier (Ivory Coast na Paris Saint-Germain), Aymen Abdennour (Tunisia na Valencia), Eric Bailly (Ivory Coast na Manchester United), Joyce Lomalisa (DR Congo na AS Vita)
Viungo: Khama Billiat (Zimbabwe na Mamelodi Sundowns), Rainford Kalaba (Zambia na TP Mazembe), Keegan Dolly (Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns)
Washambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Riyad Mahrez (Algeria na Leicester City)

12. Tuzo ya Kiongozi Bora wa Soka (Football Leader of the Year): Manuel Lopes Nasciment, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Guinea Bissau (GBFF)

13. Tuzo ya Heshima ya CAF (CAF Platinum Award): Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari kutokana na mchango uliotukuka katika soka kwa mwaka wa 2016

14. Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika (African Player of the Year): 
Mshindi wa Kwanza: Riyad Mahrez (Algeria na Leicester City)
Mshinfdi wa Pili: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund)
Mshindi wa Tatu: Sadio Mane (Senegal na Liverpool)

Cafonline.com

Mwisho


No comments:

Post a Comment

Pages