Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

YOUNG DEE-SIFIKIRII KWENDA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa kizazi kipya  nchini, David Ganzi 'Young Dee' amesema kuwa hafikirii kwasasa kufanya jitihada za kwenda kimataifa wakati bado nyumbani hajapenya ipasavyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Young Dee alisema anachoamini ni kuwa msanii hawezi kufanya vizuri kimataifa kama bado nyumbani hajafanya vizuri.

"Kuna sehemu mimi bado Bongo nahisi sijafika, Tanzania ni Nchi kubwa sana, kuna Afrika Mashariki kuna Afrika halafu ndio kuna kimataifa hivyo lazima nianze huko ndo nije kimataifa," alisema na kuongeza kuwa:

"Sijafikiria kujulikana kimataifa, lazima nianze kwanza Afrika Mashariki ili nihakikishe nimetoboa, kule watakuwa na sababu hata kunikubali kwasababu tayari nyumbani nakubalika," alisema.

No comments:

Post a Comment