HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2017

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba kwa uongozi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Beatrice Erasto,  Beatrice Erasto. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza katika hafla hiyo. 
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza katika hafla hiyo.  
  Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo.
 Baadhi ya maofisa wa CRDB pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Beatrice Erasto, akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (wa pili kushoto), 

Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akikabidhi msaada wa vifaa tiba Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Beatrice Erasto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Beatrice Erasto, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Beatrice Erasto, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

WAKATI Dunia ikiadhimisha siku ya mwanamke, Benki ya CRDB imeshiriki katika siku hiyo kwa kutoa misaada ya vifaatiba kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean road iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Shirikishi kutoka CRDB, Esther Kitoka, alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 10 utawafariji wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo.

Alivitaja vifaa tiba walivyopeleka katika hospitali hiyo kuwa ni makabati 20 yanayokaa pembeni ya vitanda vya wagonjwa, nepi za kutupa 1,500 na mifuko 1,500 maalum ya kuhifadhi haja kwa wagonjwa wanaoshindwa kujisaidia kwa njia ya kawaida.

“CRDB imejiwekea sera endelevu ya kuchagia asilimia moja ya faida yake kuchangia maendeleo ya jamii katika sekta ya afya, elimu na utunzaji wa mazingira,” alisema Kitoka.

Akiishukuru CRDB kwa msaada huu, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto alisema katika ofisi yake zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa wanaowahudumia ni wanawake wanaosumbuliwa na saratani ya kizazi na matiti.

“Msaada huu umekuja kwa wakati na mahali sahihi kabisa wagonjwa wetu wengi ni wakina mama na kama mnavyojua sisi tunategemea zaidi serikali katika kujiendesha kwetu na siku zote bajeti ya serikali huwa haitoshi.

“Tunapopata misaada kwa wadau kama CRDB na wengine ambao nawaomba wajitokeze zaidi kuwasaidia wanawake hawa… wagonjwa wetu wanakaa sana hospitali kwa sababu ya aina ya matibabu wanayotakiwa kupata,” alisisitiza Erasto.

No comments:

Post a Comment

Pages