HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2017

DC Chunya awataka wauazaji wa viroba kujisalimisha

NA KENNETH NGELESI, CHUNYA

MWENYEKITI wa kamati  ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Rehema Madusa amewataka wafanyabiashara wote walioficha pombe kali zilizofungashiwa kwenye mifuko ya plasitik maarufu ‘Viroba’ ambayo imepigwa maraufuku na Serikali wanajisalimisha kabla hatua kali hazija chukuliwa dhidi yao.

Rai hiyo ilitolewa juzi Mjini Makongorosi Wilayani Chunya mara baada ya kuendesha zaoezi la kuwa saka wafanyabiashara hao na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao wakiwa na Pombe kali ambazo zimepigwa marufuku na Serikali kupitia agizo la Waziri mkuu Kasim Majaliwa.

Katika masako huo jumla ya wafanyabioashara wannne wanashilikliwa kwa kukutwa na Pombe hizo ambao ni Nestory Filbert (23) mkazi wa Lupatingatinga ambaye alikutwa akiwa na viroba paketi 9849 aina ya Shujaa na paketi 100 za Konyagi Jackson Elias (55) mkazi wa Makongolosi akiwa viroba paketi 225 aina mbalimbali.
 

Wengine Filbert Kalumanzila (60)mkazi wa Makongolosi Wilaya ya humo ambaye alikuwa na pombe hiyo akiwa na viroba paketi 240 aina ya Ridder zinazo toka nchi ya Malawi, na Joshua Mwakaja (42) mkazi wa Makongolosi akiwa na pombe kali viroba paketi 100 aina ya ridder na Gun 165 na chupa za ridder 60.

Mkuu huyo aliongeza kuwa mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ni Joyce Bathlomeo (36) Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaoni Wilayani humo alikamtwa akiwa na pombe na viroba vya aina mbalimbali ambavyo ni “high life”  paketi 180 na aina ya Fiesta paketi 450 zikiwa zinauzwa katika duka lake la jumla.

“Pombe zilizo kamatwa ni aina nyingi sana zingine ni Van Roh,
Leader’s, Players, Kahawa Fusio, Double Punch, Charger Tanzania, Bwenzi, Rider na Watuhumiwa watachukuliwa hatua za kisheria.” Alisema Madusa.

Kwa upande wake Joshua Mwaisenye mkazi Makongolosi alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia maagizo Serikali juu ya ukatazwaji wa kutumia pombe kali ambazo zimekuwa na madhara makubwa kwa vijana.

Alisema Serikali inatakiwa kuzuia mipaka yote ambayo pombe hizo aina za viroba zimekuwa vikipitishwa na kuleta madhara makubwa kwa vijana ambao ni tegemeo kubwa kwa taifa na ninguvu kazi kwa nchi.

Mwaisenye alisema pombe hizo zimekuwa zikitoka nchi ya Zambia na Malawi na kuingizwa hapa nchini lakini zimekuwa zikileta madhara makubwa zaidi kwa vijana kutokana na kuwa na kilevya kikubwa zaidi.

Mwananchi mwingine Alex Kinyamagoha alisema viroba hivyo vinavyo ingizwa hapa nchi vinaujazo wa asilimia 43 kwa pake ti moja hivyo watumiaji wakinywa zaidi ya viwili husabisha kukosa nguvu na kushindwa kufanya kazi.

“Tumewahi kushuhudia wenzetu vijana wakipoteza maisha kutokana na unyaji wa hizo pombe ambazo zimekuwa zikitoka nchi za Malawi na Zambia, na zimekuwa zikiingika kwa njia ya panya.” alisema Kinyamagoha.

No comments:

Post a Comment

Pages