HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2017

DK. HASSAN ABBAS AWAFUNDA MAAFISA HABARI WA SERIKALI

Na Atley Utonga
Serikali imesema, Maafisa habari wa Serikali kote nchini moja ya vigezo vitakavyo tumika kuwapima katika utendaji wao wa kazi ni pamoja na wingi wa taarifa watakazo kuwa wanazalisha kwenye tovuti za taasisi walipo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbas, alipokuwa akizungumza na maafisa habari na TEHAMA, wanao endelea na mafunzo ya Utengenezaji wa Tovuti katika kituo cha Dodoma, kutoka mikoa na Halmashauri za mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Dar es salaam, Pwani na Dodoma, katika Ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma.
Abbas amesema, mara baada yakukamilika kwa Tovuti, shughuli kubwa iliyopo mbele yetu nikuhakikisha tovuti hizo zinakuwa hai muda wote kwakuwekewa taarifa sahihi na kwa wakati, ili wanchi waweze kujua mambo mbali mbali kama vile kuimarisha mifumo ya mawasiliano lakini kuongeza Utawala bora na ushirikishwaji wananchi, kwakuweka taarifa zinazo hitajika kwa wananchi.
Abbasi amesema “Sifa kuu ya Ofisa Habari wa karne hii nikuwa “Proactive”, kama wewe ni Ofisa habari lakini sio Proactive huwezi kwenda na malengo tunayo kusudia, na suala kuwa Pro-active nipamoja na kuzisakanya taarifa sahihi na zenye manufaa kwa jamii yako, amesema Dkt. Abbas
Ameongeza kuwa na sifa hiyo pekee haitoshi bali pia uzingatiaji wa suala la ;muda hatuwezi kuwa “Proactive” wakuzitafuta habari lakini hatuziweki kwa wakati nilazima tunapokuwa “Proactive” suala la muda likapewa kipaumbele sio habari ziwe zilizopitwa na wakati. “Jambo limetokea leo halafu unakuja kutuwekea kwenye Tovuti baada ya wiki tatu haitatusaidia” amesema Abbas, na kuongeza sifa zingine nikuwa Mbunifu na kufanya kazi kama timu moja.
Akiunga mkono rai hiyo ya Dkt. Hassan Abbas, Dkt. Peter Kilima kutoka Mradi wa PS.3 ambao ni wafadhili wa mafunzo hayo kwa Halmashauri 93 na Mikoa 13 nchini Tanzania katika awamu ya kwanza, yeye kwa upande wake amesema, suala la ;(Team work), kufanya kazi kwa pamoja, “Kipekee nimeguswa na kauli ya mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na zaidi sana hiyo ya kufanya kazi kama timu moja” amesema Kilima.
Nao baadhi wa Washiriki wa mafunzo hayo, wameiomba serikali kuliona suala la uhaba wa ;maafisa habari waliopo kwenye mikoa na Halmashauri kwani imebainika baadhi ya Mikoa na Halmashauri nchini hazina Maafisa habari hivyo kuifanya shughuli ya uaandaji wa maudhui ya tovuti kuwa ngumu pindi wamalizapo mafunzo.
Akizungumza p;katika mafunzo hayo Bi. Janeth Mollel Ofisa Tehama wa ;Halmashauri ya Hanang, amesema, kiufupi wanaishukuru PS.3 kwa mafunzo lakini wanaiona changamoto iliyopo nikutokuwepo kwa Maafisa habari kwa baadhi Halmashauri,
Amesema p;“Mimi najaribu kufikiri katika Halmashauri ninapotoka, ipo baadhi ya mifumo ambayo natakiwa niweze kuisimamia, kama vile Epicor, Lowson, LGRPIS, PSSN, na GoT-Homic, halafu mimi huyo huyo natakiwa nikafute maudhui na kuyaweka kwenye tovuti itakuwa ni shughuli ngumu sana” amesema Janneth, huku akiwaomba TAMISEMI kufikiria namna yakutatua changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine ;Mkuu wa mawasiliano wa PS.3 Bibi Leah Mwainyakule, amesema kufikia siku ya jumatatu ya tarehe 27 Machi, 2017 Tovuti zote kutoka mikoa iliyopatiwa mafunzo zitakuwa hewani “Tutafanya uzinduzi wa kitaifa siku ya jumatatu katika Ukumbi wa Hazina hapa Dodoma kwani maandalizi yote yamekamilika, ikiwapo kupeleka mialiko kwa wadau wote na Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.George Simbachawene(MB).

No comments:

Post a Comment

Pages