HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 31, 2017

Kamati ya Bunge, Ulinzi na Usalama yapitia bajeti ya Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoji Dodoma leo

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Mhandisi Hamad Massauni,  akisoma Bajeti ya Jeshi la Magereza kwa mwaka wa fedha 2017/2018 katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Majeshi yaliyopo  katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.
Sehemu ya Makamishna wa Jeshi la Magereza na Uhamiaji wakifuatilia Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichopitia Bajeti  ya mwaka wa fedha wa 2017-2018 kwa Majeshi yaliyoko katika Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani kilichofanyika mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji, Thobias Andengenye akijibu hoja mbalimbali zilizoulizwa na wajumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Jeshi hilo katika mwaka wa fedha uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichopitia Bajeti  ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 kwa Majeshi yaliyoko katika Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dr. Juma Malewa, akitoa ufafanuzi wa shughuli zitakazotekelezwa kwenye Bajeti ya Jeshi hilo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Majeshi yaliyopo  katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, akiwa pamoja na watendaji Waandamizi wa Jeshi la Uhamiaji wakifurahia jambo wakati  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi  Adad Rajab  hayupo pichani, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kuipitia Bajeti  ya Jeshi la Uhamiaji kwa mwaka ujao wa fedha katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hatua ambayo ni muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

Pages