HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2017

Mama Samia mgeni Tamasha la Pasaka


 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya Mwenyekiti wake Alex Msama, amemtangaza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamaska la mwaka huu utakaofanyika April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini  Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuelezea maandalizi ya tukio hilo linalowaleta watu wengi bila kujali tofauti za dini zao kusikiliza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia nyimbo mbalimbali, Msama wao wamefurahi kuona Mama Samia amekubali kubeba jukumu hilo kwa mikono miwili.

Msama alisema pamoja na Mama Samia kukubali  kubena jukumu hilo lenye heshima na hadhi yake katika jamii, pia amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kumwakilisha kwani siku hiyo atakuwa nje ya nchi.

“Tunamshukuru Mama yetu Makamu wa Rais, Mama Samia kwa kukubali kubeba jukumu la Tamasha la Pasaka kwa sababu ni jambo kubwa kweyu sisi waandaaji. Kwa mikono miwili amekubali heshima hiyo, lakini kutiokana na siku hiyo atakuwa nje ya nchi, amemteua Waziri Mwigulu kumwakilisha,” alisema Msama.

Kuhusu uteuzi wa Mama Samia, Msama alisema ni mwendelezo wa utamaduni wa Tamasha la Pasaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, kualika wageni wenye hadhi na heshima yao katika jamii iwe kutoka ndani ama nje ya Serikali.

“Tangu mwaka 2000, Tamasha hili limekuwa likiwapa viongozi mbalimbali iwe kutoka ndani ama nje ya Serikali kuwa wageni rasmi katika tukio hili bila kujali tofauti ya dini nah ii ni moja ya heshima yake, hivyo musiki wa injili kupendwa na watu wote,” alisema Msama.

Alisema ingawa Tamasha la Pasaka ni tukio la kikristo kwamba ni kumbukumbu ya kufa na kufufukwa kwa Yesu Kristo ikiwa ni fumbo la ushindi wa wakristo dhidi ya dhambi, bado tangu kuanziashwa kwake tukio hili limekuwa likiwaleta pamoja watu wa dini mbalimbali.

Msama alisema kwa kutambua  heshima na hadhi ya tukio hilo, ndio maana kamati ya maandalizi imekuwa ikiteua viongozi wenye heshima na hadi yao katika jamii kuwa wageni rasmi, hivyo amewasihi wadau wa Tamasha hilo kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru.

Alisema baada ya Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kabla ya kwenda Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Iringa kwa tarehe zitakazotajwa kulingana na ratiba kamili.

Kuhusu waimbaji, Msama amesema waimbaji watatu kutoka Kenya, wamethibitisha kushiriki Tamasha hilo ambao ni mwimbaji  mkongwe, Faustine Muhishi, Danny ‘M’ na Messi Masika ambao watashirikiana na wengine waliotajwa.

No comments:

Post a Comment

Pages