HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2017

MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga (pichani), leo Jumatatu Machi 13, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaounda kikosi hicho.

Taifa Stars, inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika leo Makao Makuu ya TFF, yalioko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni     (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao  (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya    (Simba SC).

Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta       (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu    na AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu(Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

Pia Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata wakati Meneja wa timu upande wa ufundi atakuwa mwenyewe Mayanga na upande wa mipango mingine atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo   akiwa ni Gilbert Kigadya.


Timu hiyo itaingia kambini Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam na mara baada ya michezo hiyo kambi itaahirishwa Machi 29, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages