Dande Contanct

KWA MAWASILIANO ZAIDI. E-mail: dande15us@gmail.com.

CRDB

CRDB
.

UTT

UTT
.

NSSF-SHIB

.

.

Pages

MTAWA WA JIMBO KATORIKI MBINGA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI

FIKIRI KAPINGA, MBINGA          
                  
Mtawa  mmoja  wa kanisa  katoriki  jimbo  la  mbinga  mkoani  Ruvuma  amefikishwa  katika  mahakama  ya wilaya  kujibu  tuhuma  za  uwizi wa  Fedha jumla ya TSHS.M.28.8/= mali ya Jimbo .

Imedaiwa  na mwendesha  mashtaka  wa Polisi  Ast  Inspekta  SEIF   KILUGWE  mbele  ya hakimu mkazi  mfawidhi katika  mahakama  ya wilaya  mbinga  MAGDARENA   NTANDU  kuwa mtuhumiwa  Mtawa  EMANUELA  NINDI [40] wa kanisa  katoriki  Jimbo  la mbinga  amedaiwa   kutenda  makosa  hayo  mwaka  jana kwa  nyakati  tofauti  tofauti akiwa  mtunza   fedha  za Jimbo   hilo .

KILUGWE aliendelea kudai  mahakamani hapo kuwa  mtuhumiwa  EMANUELA alikuwa  anachukua  Fedha hizo  kidogo kidogo  hadi  kufikia  jumla  ya TSHS .M. 28.8/=  ambazo ni  makusanyo ya miradi  mbali mbali  ya Jimbo  pamoja  na michango  ya waumini . 

Mshtakiwa  alikana  mashtaka na  yuko mahabusu kwa kukosa  wadhamini  wawili  wenye  sifa  hadi  machi  28  mwaka huu  kesi  hiyo  itakapo  tajwa tena

No comments:

Post a Comment