Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

Mwanamitindo agongwa na treni akipigwa picha Marekani

Mwanamke wa umri wa miaka 19, ambaye alikuwa anaanza kujikuza kama mwanamitindo, aligongwa na treni na kufariki alipokuwa anapigwa picha.
Fredzania Thompson (pichani), alikuwa anapigwa picha hizo zake za mitindo, ambazo zilikuwa za kwanza, kwenye reli alipogongwa na gari moshi.
Picha za Thompson, alizopigwa muda mfupi kabla ya mkasa huo kutokea Navasota, Texas, zimesambazwa na familia yake.
Polisi wanasema alikuwa mjamzito wakati huo na kwamba alikuwa anaondokea treni moja kwenye njia moja ya reli alipojipata ameingia kwenye njia ya reli ambapo kulikuwa na treni nyingine iliyokuwa inapita ambayo ilimgonga. BBC.

No comments:

Post a Comment