HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 11, 2017

NSSF YADHAMINI MBIO ZA TULIA MARATHON

Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF limedhamini na kushiriki katika mbio za Tulia Marathon zilizofanyika mkoani mbeya Machi 11. 

Mgeni rasmi wa mbio hizo   mh. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye aliipongeza NSSF kwa kudhaamini na kuomba utaaratibu huo uwe endelevu na uimarishwe zaidi. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
Kaimu Meneja Masoko na Uhusiano, Salim Kimaro alisema SHirika lina utaratibu wa kurudisha fadhila Kwa Jamii na maeneo yao makuu ni katika ELimu, Afya, mazingira na michezo. Yote hayo yanapofanyika ipasavyo huifanya jamii iongeze tija katika uzalishaji.
 Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Willium Lutambi (kulia), akishiriki mashindano ya mbio za Kilometa 5 ya Tulia Marathon yaliyofanyika jijini Mbeya Machi 11. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Willium Lutambi (kulia), akimaliza mbio hizo na washiriki waenzake.
 Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Salim Kimaro akiwa meza kuu na viongozi wengine.
 Meza Kuu.
 Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Salim Kimaro, ambao ni mmoja wa wadhamini akitoa hotuba yake.
Kaimu Meneja Masoko na Uhusiano wa NSSF, Salim Kimaro, Salim Kimaro, akimpongeza mshindi wa mbio za Kilometa 2 za mbio za Tulia Marathon kwa Wazee, Ndemwi Kimaro, yaliyofanyika jijini Mbeya Machi 11. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya Willium Lutambi na kulia ni Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusinao, Amina Mbaga.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa NSSF.
  Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Salim Kimaro akiwa na washiriki wenzake wa mbio za Tulia Marathon.Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya Willium Lutambi (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa NSSF. Wa tatu kulia ni Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Salim Kimaro na wa tatu kulia ni Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusinao NSSF,  Amina Mbaga.
Kucheza kwaito.

No comments:

Post a Comment

Pages