HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

March 31, 2017

NSSF YATOA MSAADA WA KOMPYUTA KITUO CHA AFYA MAGOMENI DAR

Shirika la Taifa la Hifahdi ya Jamii (NSSF), umetoa msaada ya Kompyuta tano zenye thamani ya Sh. Milioni 9, katika Kituo cha Afya cha Magomeni kwa lengo la kusaidia kutunza kumbukumbu za wagonjwa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Theopista Muheta, alisema wameamua kufanya hivyo ili kusaidia wagonjwa ambao ni wanachama wao wanaotibiwa katika Hospitali hiyo kuweza kupata huduma nzuri kutokana na kuwepo na taarifa sahihi.

Alisema Hospitali hiyo ni moja ya Hospitali ambazo wanachama wao wanatibiwa kwa kiwango kikubwa hivyo wametoa Kompyuta kwa ajili ya kuwezesha wahudumu kuhifadhi taarifa hizo Kielectoniki tofauti na sasa wanavyotunza katika makaratasi.

“Wanachama wetu wengi wanatibiwa hapa, tumekuwa tukitoa msaada mbalimbali katika vituo vya afya kwasababu wafanyakazi na wastaafu wa NSSF ndipo wanapotibiwa, kunavyokuwa na taarifa sahihi huduma zinakuwa bora Zaidi” alisema Muheta.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Aziz Msuya alisema vifaa hivyo vimekuja muda muafaka kwasababu wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha kwamba taarifa zote za wagonjwa zinahifadhiwa kwa njia ya Kielektoniki.

Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitunza taarifa za wagonjwa katika makaratasi hali inayosababisha baadhi ya taarifa hizo kupotea au kuchelewa kupatikana pindi zinapohitajika.

“Tulikuwa tuna mahitaji ya Kompyuta 20 kwasasa bado 15, sasa hivi tumeanza kutoa huduma kwa njia ya elektoniki tunaomba na watu wengine wajitokeze kusaidia katika hili ili tuboreshe huduma za afya” alisema Msuya.
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista Muheta, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Kompyuta tano kwa uongozi wa Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya, akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa Kompyuta tano zilizotolewa na NSSF kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista Muheta (kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa kompyuta tano Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya (kushoto), kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho, Idd Msumagilo, Mjumbe wa Bodi, Rashid Mbatti na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magomeni Dk. Faith Rashan Mdee. 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya (kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam kutoka kwa Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Theopista Muheta.
 Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista Muheta (kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa kompyuta tano Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya (kushoto), kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo hicho, Idd Msumagilo, Mjumbe wa Bodi, Rashid Mbatti na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magomeni Dk. Faith Rashan Mdee. 

 Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista Muheta (kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa kompyuta tano Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya (kushoto), kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya (kushoto), akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa Kompyuta tano kutoka NSSF kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
 Ofisa Uhusiano na Masoko wa NSSF, Kiamba Rajab, akizungumza na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dk. Aziz Msuya, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Kompyuta tano zilizotolewa na NSSF kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam.
Komyuta zilizotolewa na NSSF kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magomeni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages