HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2017

Polisi kuwakamata waishio mabondeni

Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuanzia sasa linaanza kuwakamata watu wanaoishi mabondeni pamoja na familia zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema amewaagiza makamanda wa polisi wa mikoa (OC- CID) kupita maeneo ya mabondeni hasa katika bonde la Msimbazi.
Alisema watu wawili akiwamo mtoto wa miaka 13, Imelda Ngonyani, mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Mongo la Ndege wamepoteza maisha kutokana na mvua zilizonyesha siku tatu zilizopita na kusababisha kusombwa na maji.
Sirro alisema mwanafunzi huyo alikufa maji baada ya kujaribu kuvuka Mto Msimbazi wakati akielekea shuleni. 
Katika hatua nyingine, Sirro alisema ametoa maagizo kwa polisi wake kuacha kumwaga vyakula katika baa zinazofanya biashara usiku hata kama wamevunja sheria.
“Nimetoa maelekezo kwa askari baada ya kupata malalamiko kutoka kwa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba askari wanamwaga vyakula katika baa mbalimbali hapa jijini,” alisema Sirro.

No comments:

Post a Comment

Pages