HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2017

PROF.GABRIEL AMEWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI KUJIONGEZEA UWEZO WA KITAALUMA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Maafisa Mawasiliano wakati wa ufungaji wa Kikao kazi kwa Maafisa hao kilichofanyika Mjini Dodoma. (Picha zote na Raymond Mushumbusi-WHUSM Dodoma).
 Pix 4 Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Paschal Shelutete akitoa neno la Shukrani kwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa Kikao kazi kwa Maafisa hao kilichofanyika Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa vyeti kwa kwa wadhamini kutoka TSN, TTCL, Multichoice Tanzania, TANAPA, SSRA mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kilichofanyika Mjini Dodoma.

Na Lorietha Laurence

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kujiongezea uwezo wa kitaaluma  ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii  na kushirikiana na vyombo vya habari katika  kuisemea serikali ili kufanikisha dira ya mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John  Kijazi wakati akifunga kikao  kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Mkoani Dodoma. 

“Ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini kwenda na wakati hasa wakati huu wa mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuendana na kasi ya utoaji wa taarifa kwa haraka na hivyo kuondoa suala la sintofahamu kwa wananchi kuhusu shughuli zinazofanywa  na serikali” alisema Prof.Gabriel.

Prof.Gabriel aliongeza kwa kutoa wito kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuchukua yale waliojifunza katika kikao kazi hicho na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo ili kuweza kuimarisha utendaji wa shughuli ya mawasiliano ya serikali kwa umma.

 Aidha Katibu Mkuu Prof. Gabriel aliipongeza Idara ya Habari Maelezo chini ya Mkurugenzi Hassan Abbas kwa kazi nzuri waliofanya ya kuandaa na kusimamia kikao kazi hicho ambacho kimekuwa chachu ya kuwakumbusha Maafisa Habari majukumu yao .

“Napenda pia kuchukua fursa hii kuipongeza Idara ya Habari Maelezo kwa kazi nzuri ya kuandaa kikao kazi hiki ikiwa ni mpango makakati mzuri wa kuandaa mawasiliano ya kimkakati kwa ajili ya kuhabarisha umma “alisema Prof.Gabriel.

Kwa upande  wake  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Nuru Millao Mwenyekiti wa kikao kazi hicho alieleza kuwa  amefurahishwa na majadiliano na mipango mizuri iliyoazimiwa na   Maafisa  Mawasiliano kwa kuwa ni jukwaa la mafunzo ya kupeana uzoefu kwa lengo la kuimarisha mawasiliano serikalini.

Naye Mwenyekiti mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw.Paschal Shelutete ameahidi  kufanyi kazi kwa bidii kwa kuhakikisha shughuli zinazotekelezwa na serikali zinaufikia umma kupitia vyombo vya habari nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages