HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2017

Rais TCCIA awashika sikio Kagera, Mwanza

 Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Ndibalema Mayanja, akizungumza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara jijinMwanza. Kushoto ni mshauri wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Lazzaro Kiheya na kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Mwanza, Leonard Lema. (Na Mpiga Picha Wetu). 

Mshauri wa Chama cha Wafanyakazi wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoa wa Mwanza, Lazzaro Kiheya, akizungumza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara uliofanyika jijin Mwanza juzi. Kulia ni Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Ndibalema Mayanja. (Na Mpiga Picha Wetu).
 NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Ndibalema Mayanja, amewataka wafanyabiashara wa Mikoa ya Mwanza na Kagera kuchangamkia soko la awali la hisa za TCCIA Investment PLC.



Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa mikoa hiyo, Mayanja  alisema, TCCIA Investment PLC,  ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na inayofanya vizuri.

Alisema, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, wakati huo ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97, imepiga hatua kubwa.

Mayanja alisema, TCCIA imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 huku ikiendelea kulipa gawiwo kwa wanahisa wake.

Rais huyo alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi wa mikoa hiyo umuhimu wa kuchangamkia fursa hiyo muhimu na adhimu.

“Muitumie vizuri fursa hii  kabla ya Machi 14,” alisema Mayanja.

Akiwa katika ziara hiyo ya mkoa wa Mwanza na Kagera, Mayanja pia alifanya kazi ya kujenga uhai wa chemba kwa kukutana na viongozi mbalimbali katika mikoa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages