HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 16, 2017

SAFARI YA MWISHO YA SIR GEORGE KAHAMA

 Mama Janeth Kahama akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mume wake marehemu, Sir George Kahama wakati wa ibada iliyofanyika katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo, kabla ya mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande). 
 Mwili wa Sir George Kahama wakitolewa katika Kanisa la St. Peter na kuelekea katika makaburi ya Kinondoni.
  Waombolezaji wakisindikiza mwili wa Sir George Kahama, wakati ukitolewa katika Kanisa la St. Peter na kuelekea katika makaburi ya Kinondoni.
  Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Sir George Kahama, wakati wakielekea katika makaburi ya Kinondoni. 
 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, akitoa salama za rambirambi wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Sir George Kahama, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mawaziri Wakuu wastaafu wakiwa katika ibada ya kuaga mwili wa aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali marehemu Sir George Kahama kutoka kulia ni Edward Lowassa, Cleopa Msuya na Fredrick Sumaye.
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akitoa pole kwa familia ya marehemu, Sir George Kahama.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili Sir george Kahama, ambaye  aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kabla ya kustaafu, wakati wa ibada ya kuaga mwili jijini Dar es Salaam. 
Mjane wa marehemu Sir George Kahama akitoa heshima za mwisho.
 Mwili ukiwasili makaburini.
 Mwili ukiwekwa kaburini.
 Mjane wa marehemu Sir George Kahama akiweka mchanga katika kaburi la mume wake.
 Akiweka maua.
 Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na mkewe wakiweka mchanga katika kaburi la Sir Kahama.
 Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, akiweka udongo.


No comments:

Post a Comment

Pages