HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2017

SAMATTA ATUPIA 2 STARS IKIICHAPA BOTSWANA 2-0

Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa),  wao dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. (Picha na Francis Dande).
Wachezaji wa Stars wakisalimiana na wenzao wa Botswana.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisson Mwakyembe, akisalimia na nahodha wa Stars, Mbwana Samatta.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisson Mwakyembe, akisalimia na nahodha wa Stars, Mbwana Samatta. 
 Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta, akimtoka beki wa Botswana, Ofentse Nato, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa (Fifa), uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 


Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta, akimtoka beki wa Botswana, Ofentse Nato.

Kipa wa Botswana, Kabelo Dambe, akiruka bila mafanikio kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na kuhesabu bao la pili kwa timu yake katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na (Fifa).
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta (katikati), akishangilia bao la pili aliloifungia timu yake bao la pili. 
 Aliyekuwa Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiagana na mashabiki wa soka waliofika kushuhudia pambano la timu ya soka ya Tanzania na Botswana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars ilishinda 2-0.

 Asanteni sana.......

No comments:

Post a Comment

Pages