HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2017

Shusho, Mwaipaja ndani ya Pasaka

.Viingilio ni shilingi 10,000; sh 5,000 na sh 3,000

NA MWANDISHI WETU

WARATIBU wa Tamasha la Pasaka litakalozinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kisha kuhamia mikoa minne, wametaja waimbaji wengine wawili watakaopamba tukio hilo la kimataifa pamoja na viingilio.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kwamba waimbaji hao wawili wanafanya idadi yao ifikie watatu hadi sasa, baada ya wiki iliyopita kumtaja Jesca Honoli ‘Jesca ‘BM.’

Waimbaji hao waliotajwa jana ni Christina shusho aliyewahi kutamba na vibao mbalimbali kikiwemo Unikumbuke pamoja na Martha Mwaipaja ambaye pia anatamba na nyimbo mbalimbali kali.

“Tunashukuru maandalizi ya Tamasha letu yanaendelea visuri sana, waimbaji wamezidi kuthibitisha kumwimbia Mungu. Baada ya Jesca BM, wengine ni Christina Shusho na Martha Mwaipaja,” alisema Msama.

Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kupitia uratibu wa matasha ya injili, alisema kuthibitisha kwa waimbaji hao nguli ni mwanga zaidi kwa tukio hilo litakalowaleta waimbaji wa ndani na nje ya nchi.

Alisema tukio hilo ambalo hadi sasa maandalizi yake yanakwenda vizuri kwa asilimia 90, hasa baada ya kupata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kiingilio ni sh. 10,000 kwa viti maalumu, sh 5,000 kwa watu wakubwa na shilingi 3000 kwa watoto.

Kuhusu mikoa  itakayoshambuliwa na Tamasha hiyo, Msama alisema mikoa iliyopitishwa na Kamati yake, ni Dar es Salaam (April 16), Dodoma (April 17) kabla ya kuhamia Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza hapo April 23.

Msama alisema kwa vile mipango ya Kamati yake ni kuifikia mikoa mitano, baada ya uzinduzi wa April 16, baada ya Dodoma na Mwanza, mikoa mingine mitatu itajulikana baadaye kwa vigezo kwa  mujibu wa vigezo mbalimbali.
Alisema malengo ya msingi wa tamasha hilo linalofanyika mara ya 17 tangu kuasisiwa kwake mwaka 2000, yanabaki ni kueneza ujumbe wa neno la Mungu kwa mataifa yote na kufariji makundi maalumu kama yatima, wajane na walemavu.

Msama alisema anaamini tamasha la mwaka huu litakalofanyika chini ya kaulimbiu ya Upendo, Umoja na Mshikamano wa Watanzania, hujenga Taifa Imara, litakuwa lenye ubora wa hali ya juu tofauti na mengineyo kadhaa yaliyowahi kufanyika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akifafanua jambo.

No comments:

Post a Comment

Pages