HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2017

MGWATU AWAAGIZA WATUMISHI KUZIBA MIANYA YA UVUJAJI MAPATO VIVUKO VYA KIGONGO-BUSISI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akijibu swali la mmoja wa wafanyakazi wa vivuko vya Kigongo/ Busisi wakati alipokua akisikiliza changamoto na kero zinazowakabili wafanyakazi wa vivuko hivyo. Pembeni yake ni Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dokta Mussa Mgwatu akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa vivuko vya Kigongo Busisi vinavyomilikiwa na TEMESA mkoani Mwanza wakati wa kikao chake na wafanyakazi hao. Kushoto kwake ni Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo, Mhandisi Michael Myaka na Mkuu wa vivuko Atiki Abdalah.
Wafanyakazi wa Vivuko vya Kigongo-Busisi vinavyomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Dkt. Mussa Mgwatu hayupo pichani wakati alipokua akizungumza nao kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika mazingira ya kazi zao kivukoni hapo.
Mmoja wa Manahodha wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Kelvin Willy akimuuliza swali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (hayupo pichani) wakati alipokua akisikiliza kero za wafanyakazi hao kivukoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu aliyeshika kitabu akiagana na baadhi ya watumishi wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya Kigongo-Busisi mara baada ya kumaliza kikao na watumishi hao jijini Mwanza. Picha zote na  Alfred Mgweno - TEMESA.

No comments:

Post a Comment

Pages