HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2017

Tamasha la Pasaka kufanyika Uwanja wa Uhuru

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.

NA  Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions  inayoratibu Tamasha la kimataifa la Muziki wa injili  tangu mwaka 2000, imesema maandalizi ya tukio la mwaka huu yanakwenda vizuri ambapo tukio la mwaka huu litafanyika katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo , Alex Msama alisema baada ya uzinduzi huo kufanyika Aprili 16 katika Uwanja wa Uhuru, litahamia mikoa 10 ambayo itateuliwa na kamati ya maandalizi.

“Nichukue fursa hii kuwatangazia wadau wa Tamasha la Pasaka na muziki wa injili kwa ujumla wake kwamba, tamasha la Pasaka lipo kama kawaida na litaanzia jijini Dar es Salaam April 16, kabla ya kwenda mikoani,” alisema Msama.

Kuhusu uteuzi wa uwanja wa Uhuru, Msama alisema hiyo ni kutokana na uamuzi wa Kamati ya maandalizi kuangalia vigezo mbalimbali yakiwamo maoni ya wadau wakubwa wa muziki huo.

“Tunaamini Uwanja wa Uhuru (zamani Taifa), ni mahali muafaka baada ya kujiridhisha kwa vigezo vingi. Tunaamini hata wadau, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili wataukubali,” alisema.

Juu ya kukawia kwa maandalizi tofauti na miaka mingine, Msama alisema ni kusubiri mambo mengine muhimu yakamilike, ikiwemo taratibu husika kwa mujibu sheria za nchi.
Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd, alisema mikakati ya Kamati yake ni kuhakikisha tamasha la mwaka huu linakuwa bomba zaidi kwa kuongeza vionjo muhimu tofauti na miaka mingine.

Kuhusu maudhui, Msama alisema mbali ya kuutukuza ufalme wa Mungu kwa njia ya nyimbo na kutumia sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu kama yatima, wajane na walemavu, pia litahimiza upendo na amani katika nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages