HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2017

Tigo, Malvik wageukia huduma bima ya afya

 Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya BimaMkononi. Kushoto ni Meneja wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin.
 Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya BimaMkononi.
Meneja wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin, akifafanua jambo katika uzinduzi wa bima ya afya ya BimaMkononi. 
 Mmoja wa wanufaika wa huduma ya bima ya afya ya BimaMkononi akizungumza.
 Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel, wakati wa uzinduzi wa BimaMkononi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mnufaika wa Huduma ya Bima ya Afya  inayotolewa na kampuni ya Tigo, Hawa Ramadhan akitoa maelezo ya namna alivyonufaika na huduma hiyo wakati wa uzinduzi wa Bima Mkononi uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel. (Picha na Francis Dande).


NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Milvik inayoongoza kwa bima ndogo nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi katika kutoa huduma za bima ya afya, imejipanga kuleta mageuazi makubwa katika sekta ya ndani ya  bima  kupitia mfumo wa TigoPesa.

Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni Milvik, zimeingia makubaliano ya kutoa Huduma hiyo tangu mwaka jana kwa kutoa Huduma ya bima kwa simu za mkononi maarufu kama Bima Mkononi inayotoa bidhaa za kipekee.

Bidhaa hizo za hali ya juu, ni kama bima ya maisha, ugonjwa na ajali kwa wateja wanaotumia Huduma ya TigoPesa, ikiwa na wateja hai zaidi ya 200,000.

Hawa Ramadhani, mama wa watoto watatu  kutoka wilaya ya Kibaha, mkoa wa Pwani,  ni mmoja wa wanufaika wa BimaMkononi anaeleza mengi kuhusu manufaa ya program hiyo katika kusaidia wananchi kupitia Tigopesa.

Akieleza jinsi BimaMkononi  ilivyobadilisha maisha yake, anasema: “Nilikuwa nimelazwa katika Hospitali ya Tumbi kwa siku 21, baada ya kuruhusiwa kutoka, niliwasilisha  taarifa za hospitali katika duka la Tigo la huduma kwa wateja na nilifurahi waliponiita baada ya siku tatu  na kupokea  kitita cha 840,000/-

Alisema,   baada ya kuitwa alielezwa kuwa bima  imemfidia kwa kipindi  alichokuwa amelazwa hospitalini.

“Kwa pesa hizo niliweza  kulipia ada ya shule ya watoto iliyokuwa imebaki, pamoja na kukuza  biashara yangu ndogo,” alisema na kutoa ushauri kwa wengine kujiunga  na mpango huo  ili wafurahie manufaa yake.

Naye Melikizedeki Nyalufujo, mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia cha St. John,  Dar es Salaam, alisema anajisikia furaha kuwa mnufaika wa BimaMkononi, baada ya kupokea 86,000/- kufuatia kulazwa kwake hospitalini kwa siku mbili kutokana na jeraha alilolipata.

“Mara ya kwanza nilipoelezwa kuhusu BimaMkononi nilikuwa na wasiwasi, lakini nilijiunga. Hata hivyo, nilishawishika kujiunga baada ya kupokea fedha hizo ndipo  nilithibitisha kwamba ilikuwa ni kweli.

“Ankara za hospitali  ilikuwa ni 16,000/-; hivyo kwa fedha  hii ya ziada  niliweza kulipia  gharama nyingine  kama vile kujikimu  chuoni, kununia vifaa  vya masomo na kulipia baadhi ya madeni madogo ambayo nilikuwa nimekopa  hapo awali. Naishukuru mno BimaMkononi,” alisema Nyalufujo kwa furaha.

Kwa mujibu wa Meneja wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin, huduma ya BimaMkononi imetengenezwa makusudi kutoa bidhaa za Bima kwa Watanzania wote ambao wanaihitaji  ambao kinyume cha hapo,  wasingeweza  kumudu huduma hiyo.


BimaMkononi, ni mfumo mpya wa bima kwa Watanzania wa kawaida ambayo inawawezesha kuwakinga dhidi ya matukio yasiyotarajiwa yanayoweza kuwa na athari kwa hali ya kifedha kama wasingekuwa wamejiunga na huduma hiyo.  Tayari BimaMkononi ishalipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 27 katika miezi sita iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Pages