Dande Contanct

KWA MAWASILIANO ZAIDI. E-mail: dande15us@gmail.com.

CRDB

CRDB
.

UTT

UTT
.

NSSF-SHIB

.

.

Pages

UCHAGUZI TAFCA KINONDONI

Kamati ya Utendaji ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni inakutana Jumamosi (Aprili 1, 2017) kupata tarehe ya uchaguzi mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Mbwana Makata (0655520129), Mkutano huo wa Kamati ya Utendaji ya TAFCA Kinondoni utaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Eliutery Mholery (0715621667).

Alisema mbali ya ajenda hiyo, pia Kamati hiyo itaanda taarifa ya utendaji pamoja na taarifa ya fedha ambazo zitawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kawaida wa chama hicho kabla ya ajenda ya uchaguzi.

Makata alisema pia Kamati yao itajadili uhai wa wanachama wao, hivyo kuwataka ambao hawajalipa ada za uanachama kufanya hivyo haraka ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Alisema makocha wote wa Kinondoni ambao ndiyo wanachama wa chama hicho wanatakiwa kulipia ada zao kupita TAFCA Taifa au kwa Mhazini wa TAFCA Kinondoni.

IMETOLEWA NA TAFCA KINONDONI 

No comments:

Post a Comment