HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2017

UJUMBE MZITO KUTOKA CHINA WAWASILI DAR ES SALAAM, LEO

NA IRENE MARK
MAKADA 19 wa Chama cha Kikomunisti (CPC) kutoka China wakiongozwa na Guo Jinlong, wamewasili nchini kwa ziara ya kisiasa na kupokelewana wenyeweji wao Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya ugeni huo kuwasili, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, alisema wageni hao watajadili masualambalimbali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Alisema leo wageni hao watakutana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dk. John Magufuli kisha watakwenda Zanzibar kwa ajili ya kuzungumza na Rais Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya kurejea Bara.

‘‘Lengo la ujio huo ni kuimarisha mahusiano baina yao na sisi hasa kwenye sekta ya uchumi na siasa mnajua kwamba China ni taifa kubwa pia ni marafiki zetu wa siku nyingi,ziara hii ni wmendelezo wa urafiki na udugu wetu, tunaimarisha pia mahusiano yetu,’’ alisema Mpogolo.

Kabla ya ziara hiyo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema CPC iliahidi kwa kushirikiana na CCM watajenga chuo cha uongozi kwa ajili ya makada wao.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, alipowasili na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, baadaya kumookea na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Pages