Dande Contanct

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU.

CRDB

CRDB
.

Pages

Christopher Mgaya aibuka na milioni 10 za Biko

Msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya kwanza ya Sh Milioni 10 ya Biko ambapo mkazi wa Temeke Christopher Mgaya, aliibuka mshindi wa kwanza wa bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Juhudi Ngolo akishuhudia.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya kwanza ya kuwania sh Milioni 10 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki imempatia donge nono mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya na kuweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kujinyakulia kitita hicho kutoka kwa mchezo wa bahati nasibu wa Biko.

Droo hiyo ilichezeshwa na msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba jumla ya washindi 2000 walipatikana katika zawadi mbalimbali, huku Mgaya yeye akiibuka kinara wa Sh Milioni 10.

Heaven alisema kwamba baada ya kupatikana kwa mteja huyo, taratibu za kumkabidhi hundi yake ya Sh Milioni 10 unaweka ili mteja huyo apate fedha zake haraka iwezekanavyo.

Tumeanza vizuri kwa kufanikiwa kumpata mshindi wetu wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambapo alicheza bahati nasibu yetu, huku yeye akifanikiwa kuibuka mshindi.

Utaratibu ni ule ule kwasababu kila mtu anaweza kushinda kwa kuinguza muamala kwa Tigo Pesa, MPESA na Airtel Money ambapo ataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kwenye kipengele cha lipa bili, huku pia akiingiza namba ya 2456 kama namba ya kumbukumbu ambapo Sh 1000 atakayocheza itampatia tiketi mbili za kushinda hapo hapo au tiketi ya kumuingiza kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10, Alisema Heaven.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo alisema kwamba wameikagua kampuni ya Biko na kuvutiwa na utaratbu wa mchezo wao, hali inayoonyesha kwamba Watanzania wapo salama katika kucheza mchezo huo.

Nimekuwa mwakilishi wa kwanza kutoka Bodi kusimamia wakati wa kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo naamini Watanzania wataamua kucheza zaidi.

Naye Mgaya mshindi wa bahati nasibu hiyo ya Sh Milioni 10 alisema haamini kwamba ameshinda Sh Milioni 10 hadi hapo atakapokabidhiwa kitita chake ingawa kimemfanya avuje jasho wakati anatangazwa yeye ndio mshindi.

Nimefurahishwa sana na kushinda kwangu mshiko wa Biko wa Sh Milioni 10 ambapo siamini kama nimeshinda zawadi hiyo kubwa kutoka kwenye kampuni ya biko.

No comments:

Post a Comment