HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 23, 2017

Mtanzania Alphonce Simbu anyakua nafasi ya 5 London Marathon

Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake, Mary Keitany (KEN) - 2:17:01.
  • Mshindi wa kwanza kwa upande wa walemavu, David Weir akimaliza mbio. 
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume, Daniel Wanjiru (KEN) - 2:05:48 
Mshindi wa pili kwa upande wa walemavu, Manuela Schar


Balozi wa DStv na Mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyeshiriki mashindano ya London Marathon yaliyofanyika leo jijini London ameibuka mshindi wa tano huku akivunja rikodi yake kwa kutumia muda wa 2:09.10 ambao ndio muda wake bora zaidi tangu aanze kushiriki mashindano ya kimataifa. Kabla ya hapo rekodi yake ilikuwa muda wa 2:09.21 aliyoiweka mwaka jana kwenye mashindano ya Lake Biwa Marathon nchini Japan.

Simbu ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon ameonyesha umahiri mkubwa katika mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni wakiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele  wakenya Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.

Mara baada ya ushindi huo salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika huku mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akisema kuwa kampuni yake imeridhishwa sana na ufanisi aliouonyesha katika mashindano hayo. Amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa matunda kwani kiwango cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku. “Tumefurahishwa sana na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London Marathon. Hii ni ishara nzuri sana na tunaamini atafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London mnamo mwezi Agosti mwaka huu”

Kwa upande wake, meneja wa mwanariadha huyo Francis John amesema kuwa ameridhishwa na kiwango alichoonyesha Simbu na kwamba punde tu atakaporejea wataanza maandalizi kwa ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika mwezi agost mwaka huu.

Katika mashindano hayo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya Danie Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan Karoki (2:05:41).

Washindi kumi bora kwa upande wa wanaume

  1. Daniel Wanjiru (KEN) - 2:05:48
  2. Kenenisa Bekele (ETH) - 2:05:57
  3. Bedan Karoki (KEN) - 2:07:41
  4. Abel Kirui (KEN) - 2:07:45
  5. Alphonce Simbu (TAN) - 2:09:10
  6. Ghirmay Ghebreslassie (ERI) - 2:09:57
  7. Asefa Mengstu (ETH) - 2:10:04
  8. Amanuel Mesel (ERI) - 2:10:44
  9. Javier Guerra (ESP )- 2:10:55
  10. Michael Shelley (AUS) - 2:11:38

No comments:

Post a Comment

Pages