HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2017

Mwaitege, Kilahiro ndani ya Pasaka Uwanja Uhuru

NA MWANDISHI WETU
HATIMAYE Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege, amethibitisha kushiriki tamasha la Pasaka litakalofanyika April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Mwaitege aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Utamtambuaje kama ameokoka, Mama ni Mama na nyingine nyingi matata, atapanda jukwaani siku hiyo pamoja na waimbaji wengine wa ndani na nje.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa, Mwaitege amethibitisha pamoja na Upendo Kilajiro, mmoja wa waimbaji mahiri wa kike nchini.
Alisema kwa waimbaji wa ndani, hao ndio wa mwisho tayari kushirikiana na wengine waliotajwa awali akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, Martha Mwaipata na Jesca ‘BM na Kinondoni Revival Choir’.
Msama aliitaja pia kwaya ya Vijana KKKT ya Tabata ambayo itatumbuiza katika tamasha hilo na kusema ni katika kutoa nafasi kwa kwaya chipukizi kupata uzoefu zaidi katika huduma hiyo.
Katika hatua nyingine, Msama alisema awali, baada ya uzinduzi wa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, uhindo huo ulikuwa uende Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma, lakini sasa hawatakwenda mkoani huko.
Alisema ingawa Kamati yake ilipenda wadau wa mkoa huo wapate uhondo wa tukio hilo, lakini hawatakwenda huko kutokana na kukosa nafasi kwa siku ambayo wangekuwa huko.
Kwa mabadikilo hayo, Msama alisema baada ya tamasha hilo kutikiza katika Uwanja wa Uhuru, jijini  Dar es Salaam, April 22 itakuwa zamu ya wadau na wapendwa wa Simiyu na siku April 23, itakuwa zamu ya wadau wa Mwanza.
Alisema wakiwa jijini Mwanza, tukio hilo litafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo mgeni atakuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.

No comments:

Post a Comment

Pages