HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 23, 2017

PICHA ZA MBUNGE BASHE JIMBONI KWAKE NZEGA

Na Dixon Busagaga,Moshi.
KAMATI ya Mashindano ya Mei Mosi ,imeonya timu za Mashirika kutumia wanamichezo wasio watumishi (Watumishi Bandia ) katika mashindano hayo huku ikitangaza kutoa adhabu kali kwa taasisi ama mashirika yatakayobainika kuwatumia wachezaji hao.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambayo hufanyika katikamkoa ambao siku kuu ya Wanyakazi Duniani hufanyika kitaifa, timu zitakazo bainika kufanya udanganyifu zitafikwa na rungu la kufungiwa mwaka mmoja kutoshiriki mashindano hayo pamoja na faini ya kiasi cha sh 500,000.
Mbali na adhabu hiyo kwa timu iliyofanya udanganyifu ,pia viongoz wa timu husika watafungiwa kwa muda wa miaka miwili kushiriki mashindano ya Mei mosi ,adhabu itakayoenda sambamba na nakala ya barua kwa waajili wa viongozi hao ya kuonesha namna watumishi hao si waaminifu.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCu) baada ya kuzinduliwa jana ,Hawad Safari  alisema ili kutoa uhakiki kamati imetoa maelekezo kwa wanamichezo wafike na vitamburisho vya kazi,Fomu inayoonesha mshahara pamoja na kadi ya bima ya afya.
Alisema mashindano hayo yanahusisha timu kutoka katika mashirikisho manne ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Uma (SHIMUTA),Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI ) ,BAMATA na Shirikisho la Michezo  Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Safari alisema hadi sasa jumla ya timu 14 kutoka taasisi na mashirika mbalilimbali zimewasili mjini hapa kwa ajili ya kushindana katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,Netiboli,Kuvuta kamba ,Mbio za baiskeli ,Marathoni pamoja na michezo ya jadi kama Bao ,Drafti na Karata.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliotanguliwa na maandamano kwa timu shiriki,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba alisema zipo taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi na mashirika wamezuia kushiriki michezo hiyo licha ya kwamba timu zao zilikwisha fanya maandalizi.
“Nivitake vyama vyama vya wafanyakazi kufuatilia suala hili ,kwa nini wafanyakazi hawashiriki katika michezo hasa hii ya Mei Mosi Kitaifa ….nchi yetu imekuwa haipigi hatua kwenye eneo hili ni kwa sababu ya viongozi hawa wasiopenda michezo mahala pa kazi”alisema Warioba.
Awali akitoa hotuba yake Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Joyce Benjamini alisema Mashindano hayo yamelenga kuongeza ushirikiano mwema kwa wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi huku akitoa rai kwa viongozi kutenga bajeti kwa ajili ya mashindano hayo.
Timu zinazo shiriki mashindano hayo ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi,Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makao –CDA Dodoma,Ofisi ya Rais Ikulu,Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Timu nyingine ni Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU),Halimashauri ya wilaya ya Hai,Halmahauri ya wilaya ya Moshi ,Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Ofisi ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Geita Gold Mining,Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na TAMISEMI.

Katika michezo ya awali timu ya soka ya TPDC ilifanikiwa kuchomoza na ushindi baada ya kuiadhibu timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa bao moja kwa sifuri huku timu ya Chuo Kikuu cha Ushirika ikitakata mbele ya timu ya Ras –Kilimanjaro kwa jumla ya ba 2 kwa 1.

No comments:

Post a Comment

Pages