HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2017

Rose Muhando kuzindua ‘Jitenge na Ruth’ Pasaka

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru. 

Na Mwandishi Wetu

ALBAMU mpya ya ‘Jitenge na Ruth’ ya malkia wa muziki wa injili kwa uakanda wa Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, ndiyo itampandisha jukwaani katika Tamaka la Pasaka la mwaka huu.

Muhando, mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini ambaye amekuwa akishiriki mara kwa mara tukio hilo hata kuwa alama ya mafanikio ya muziki huo, atalitumia Tamasha hilo kuzindua kazi hiyo mpya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema albamu hiyo yenye nyimbo kibao, itazinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru.

Msama alisema tukio la uzinduzi wa albamu hiyo na ile ya ‘Ngome Zimeanguka’ ya Kinondoni Revival, anaamini Tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti.

“Malkia wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando atakuwepo katika Pasaka ya mwaka huu akizindua albamu yake ya ‘Jitenge na Ruth,’ wadau wajitokeze kwa wingi,” alisema Msama.

Alisema uwepo wa Rose, Kinondoni Revial Choir, Kwa ‘Viumbe Vyote’ ya Tabora na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na wengine mahiri, ni faraja kubwa kwa wadau wa Tamsha hilo.

Msama alisema, baada ya uzinduzi wa nguvu katika Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Alisema wakati uzinduzi wa Uwanja wa Uhuru akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Mchemba atakayemwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mgeni katika Uwanja wa Jamhuri, ni Naibu wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavumde.

Msama alisema baada ya Tamasha hilo kutikisa vilivyo katika  Uwanja wa Jamhuri mbele ya Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, litahamia katika jiji la Mwanza, Simiyu na Iringa.

Alisema kamati yake imeamua kuufikia mji wa Dodoma kutokana na watu wake kulipenda Tamasha hilo, pia heshima ya Dodoma kama mji mkuu wa  chi na makao makuu ya serikali.

Alisema pamoja na mambo mengine yanayokwenda na tukio hilo, malengo ya msingi ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu, pia kutumia sehemu ya mapato kufariji watoto yatima, walemavu na wajane.

No comments:

Post a Comment

Pages