HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 05, 2017

SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA MAJI CHALINZE

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.


Na Raymond Muahumbusi WHUSM  Dodoma.

Serikali kwa kushirikiana na  Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirka wa Maendeleo (DPS), na Serikali ya India  kwa pamoja wametoa jumla ya Shillingi Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Chalinze kwa awamu tatu.

Akijibu Swali Mbunge wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete lililouliza kuwa Wakazi wa Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze?

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge ameeleza kuwa Serikali ipo katika utekelezaji wa mradi huo na gharama za utekelzaji wake ni Shillingi Billioni 23.4 kwa awamu ya kwanza na Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili ya mradi na kwa awamu ya tatu itagharimu Shillingi Billioni 86.9.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji umekamilika na kwa awamu ya pili ya mradi huo jumla ya vijiji 88 vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi wote waishio katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.

“Mradi upo katika hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ipo katika utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya maji” alisisitiza Mhe. Lwenge.

Pia ameleza kuwa katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi, Lulenge, tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa majaribio ya bomba kuu.

Vijiji vitatu vya Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata maji mara baada ya mkandarasi kufanya maboresho ya pampu ambazo zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa  na mkandarasi huyo ameagizwa kuhakikisha pampu  hizo zinafanya kazi kabla ya Juni 2017.

Aidha kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huu kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115), Ujenzi wa mfumo wa manomba ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki makubwa 19 na ujenzi wa vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya kuchotea maji vinatekelzwa.

No comments:

Post a Comment

Pages