HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2017

TUZO ZA RAIS ZA MZALISHAJI BORA WA MWAKA VIWANDANI KUTOLEWA APRILI 8


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga,  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akisaini leo mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga,  kwa ajili ya udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso (kushoto), akisaini leo akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga,  wa udhamini wa Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka viwandani zitakazofanyika Aprili 8 jijini Dar es Salaam. 


Na Mwandishi Wetu

Tuzo za Raisi za mzalishaji bora wa mwaka viwandani 2016 zitatolewa tarehe 8 Aprili  mwaka 2017 katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Benki M kwa mwaka wa pili mfululizo ndiye mdhamini mkuu wa tuzo hizo.


Mkurugenzi Mtendaji wa shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) Leodegar Tenga  alisema kuwa tuzo hizo zinalenga kutambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta ya viwanda nchini katika kukuza uchumi.


Amesema kuwa kwa takribani miaka kumi na mbili mfululizo, shirikisho hili limekuwa likitoa tuzo hizo kubwa kwa wanachama wake ambao hujumuisha sekta zote za uzalishaji na huduma.


Shindano la mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kuingiza katika shindano zawadi ya matumizi bora ya Nishati. Zawadi hii pia itasaidia kuhamasisha washiriki kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia matumizi bora ya nishati viwandani. CTI, DANIDA na GIZ zimekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha usimamizi na matumizi bora ya nishati viwandani mfano, ukaguzi wa nishati viwandani uliofanywa na unaoendelea kufanywa nchini kote kwa wananachama wa CTI.


Na kwa mara ya kwanza, shindano la mwaka huu pia litashirikisha kampuni zisizo wanachama wa shirikisho hilo. “Ili kutekeleza ushauri alioutoa Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa CTI, katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mwaka jana, CTI imeamua kupanua wigo wa ushiriki kwa kualika Kampuni zisizo wanachama kushiriki ili kulifanya shindano kuwa la kiushindani zaidi” alisema.


Dhumuni kuu la tuzo hizi ni kutambua mchango wa sekta ya viwanda katika ukuaji wa uchumi, kuwavutia wawekezaji zaidi katika sekta ya viwanda, kutangaza umuhimu wa sekta ya viwanda nchini, kukuza kiwango cha biashara nk.


Bw. Tenga alitoa shukrani zake za dhati kwa Benki M kwa kushirikiana nao kama wadhamini wakuu wa tuzo hizo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Kwa upande wa Benki M, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema kuwa Benki M inatambua juhudi za serikali katika kuinua sekta ya viwanda nchini


“Sekta ya viwanda ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi hivyo tunajisikia fahari kusaidia wazalishaji wa viwanda wa ndani siyo kifedha au kuwapatia huduma za kibenki tu lakini pia kupitia shindano hili maarufu la thamani. Tuzo za mzalishaji bora ni mahali ambapo makampuni wanachama na wasio waachama wa CTI kupitia mchakato wa ushindani huinua ubora wa bidhaa wanazozalisha na huduma wanazotoa katika jamii” alisema Bi Woiso.


Tuzo za raisi za mzalishaji bora wa mwaka zilianza kutolewa mwaka 2005, ni tuzo ambazo huandaliwa na shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) katika kutambua mchango wa sekta ya uzalishaji wa viwanda nchini.


Mwishoni wa mchakato wa kupata washindi, walioshinda hupewa tuzo na mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mlezi wa Shirikisho hilo. Kwa mwaka huu, Mheshimiwa Rais atawakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.


Tuzo hizi hutolewa kwa makampuni na viwanda kuanzia vidogo, vya kati hadi vikubwa kutegemea mchango vinaotoa katika kukuza uchumi nchini. Mwaka huu hafla hii inatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Takribani 400 wakiwamo wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wenye viwanda na wataalamu mbalimbali na waalikwa kutoka katika sekta binafsi na serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages