HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 21, 2017

WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serekali katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma 21/Apr/2017 wakati wa  shughuli ya  kuaga Mwili wa Maerehemu Mheshimiwa  Dr  Elly Marko Macha  ambaye alifariki  Nchini Uingereza alipokuwa katika matibabu. Picha na PMO.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akitoa heshima  za Mwisho  katika  jeneza  la  Marehemu  Mheshimiwa  Dr  Elly Marko  Macha  Mbunge wa Viti maalumu Chadema  ambaye mwili wake ulifikishwa katika viwanja vya  Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya Bunge kuaga  21/Apr/2017  Dr Macha alifariki  akiwa katika matibabu   Nchini  Uingereza.   
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa  mkono wa pole Glory  Haika Peter (24) ambaye ni Mtoto wa Maerehemu  Mheshimiwa Dr  Ell Macha  Mbunge  viti Maalumu Chadema ,Wakati wakusindikiza  Mwili wa marehemu katika Uwanja  wa Ndege wa Dodoma.




WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.

Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.
Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.

Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.
Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, APRILI 21, 2017.

No comments:

Post a Comment

Pages