HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 23, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAELEZOTV

Na Daudi Manongi-MAELEZO

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa  katika kuitangaza Serikali.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.

“Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii  kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.

Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema  kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.

“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.

Mbali na hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano  waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.

No comments:

Post a Comment

Pages