HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2017

AZANIA TEAM YAKABIDHIWA BENDERA, VIZA, TIKETI NA VIFAA VYA MICHEZO TAYARI KWENDA ANFIELD, LIVAPOOL KUMENYANA NA MABINGWA WENGINE WA KINYAN'GANYIRO CHA STANDARD CHARTERED WAY TO ANFIELD

Viongozi wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad (kushoto), Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Mohammed Bashrahili (katikati), wakiwa na Kocha wa timu hiyo, Saleh Afifi wakati wa hafla ya kukabidhi timu hiyo, bendera tayari kuelekea Jijini Liverpool, nchini Uingereza kwa ajili ya kinyan'ganyiro hicho na mabingwa wengine duniani.
Baadhi ya wachezaji wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, wakiwa katika hafla hiyo, Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Azania Team, mabingwa wa Kombe la michuano ya Standard Chartered way to Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad (wa tatu kulia), Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Mohammed Bashrahili (wa pili kulia) na Kocha wa timu hiyo, Saleh Afifi wakiwa pamoja na wachezaji wa timu hiyo, wa hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Standard Chartered, nchini Tanzania, Juanita Mramba, akizungumza katika hafla hiyo, kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, nchini, Balozi Ami Mpungwe (katikati), wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, nchini Tanzania, wadhamini wa timu hiyo, Balozi Ami Mpungwe akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Deoniz Malinzi, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo, ya kukabidhi bendera, viza, tiketi na vifaa vya michezo kwa timu hiyo. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Balozi Ami Mpungwe.
Wachezaji wa Azania Team, wakiwa na baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke.
Nahodha wa timu hiyo, Khalid Said akielezea matumaini yake na jinsi walivyojianda kwa fainali hiyo, mashindano yatakayofanyika Uwanja wa Anfield jijini Liverpool, nchini Uingereza.
Mchezaji wa timu hiyo, Thomas Bishanga, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Mchezaji wa timu hiyo, Rajb Ally, akikabidhiwa tiketi pamoja na viza yake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa nne kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke (wa tano), Balozi Ami Mpungwe (wa tatu) wa Benki ya Standard Chartered pamoja na Mwenyekiti wa BMT, Deoniz Malinzi (wa pili kushoto) na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini.
Nahodha wa timu hiyo, Khalid Said (wa pili kushoto), akiwa ameishikilia Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mara baada ya kukabidhiwa. Wa pili kulia anayefurahi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo, akipongezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Nahodha wa timu hiyo, Khalid Said, akikabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya mashindano ya fainali hizo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini, Awadh Fuad, wamiliki wa timu hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo, Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke, Balozi Ami Mpungwe wa Benki ya Standard Chartered pamoja na viongozi wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa timu hiyo pamoja na viwanda vya kusaga nafaka vya Azania nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages