Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA KAMPENI YA MIMI NA WEWE MJINI UNGUJA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Unguja, Zanzibar akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua ya kampeni maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.


Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu wasiojiweza katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.

Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa Vyama vya siasa.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Unguja- Zanzibar
20-May-2017

No comments:

Post a Comment