HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2017

SPIKA WA BUNGE MHE.JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA KENYA LEO JIJINI NAIROBI, KENYA



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika pichani kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya Justin Muturi, Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch. Peter Msigwa. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati ya waliokaa kulia) akizungumza na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta na Makamu wake Mhe William Rutto walipokutana wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa hilo. Wengine katika picha ni Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi (kulia kwa Mhe Ndugai),Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe. Ekwee Ethuro (wa kwanza kulia),Mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Rachel Chebet.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro (wa pili kushoto). Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda (wa nne kulia), Mhe Salim Turky (wa pili kulia) na Mhe Mch.Peter Msigwa (wa kwanza kulia).
Spika wa Bunge Tanzania Mhe Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake leo Jijini Nairobi, Kenya. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko wa Bunge la nchi hiyo. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Pages