HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 30, 2017

Watanzania Wametakiwa Kuisaidia Serikali Katika Kutatua Changamoto Katika Sekta Mbalimbali-Boniface


Mdau wa Maendeleo, Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Kunguru Goba, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam



Na: Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.
Myalla amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.
"Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi," amesema.
Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais  Dk. John Pombe Magufuli katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi.
Amesema wapo wanafunzi walikuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages