HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 04, 2017

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUBORESHA BARABARA ZA MAJIJI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga.  
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro. 



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ina mkakati wa kufanya yote nchini yawe na barabara za viwango vya kimataifa na zinazopitika kwa urahisi.

“Tumeanza kujenga barabara za kisasa katika jiji la Arusha ambalo ni jiji la utalii, tutakwenda Mwanza na Dar es Salaam kwa kujenga barabara zenue njia za juu (flyovers) zikiwemo za magari na za waenda kwa miguu,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Mei 4, 2017) wakati akizumngumza na wananchi wa Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km. 14.1 ambayo itakuwa na njia nne za magari.

“Nimekuja kukagua ujenzi wa barabara hii ya Sakina hadi Tengeru lakini mkandarasi akimaliza anajenga barabara nyingine ya kilometa 42.1 na hivyo hapa Arusha tutakuwa na kilometa 56.5 za awamu ya kwanza,” alisema.

Alisema maboresho ya barabara za Jiji la Arusha yanafanyika ili kuwezesha wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na viwanda vitakapoanza kujengwa, itakuwa hawana shida ya mawasiliano.

Akizungumzia tatizo la uhaba wa ardhi aambalo lililibuliwa na mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw, Mrisho Gambo aendelee na zoezi la kuuzungukia mkoa wake ili kubaini maeneo yenye matatizo sugu.

Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri Mkuu, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga alisema ujenzi wa barabara hiyo ambao ulianza Juni 2015, unatarajia kukamilika Juni 2018.

“Ujenzi wa barara ya Sakina –Tengeru ni wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 230 ya kutoka Arusha –Holili- Taveta –Voi ambayo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 139.34. Ujenzi huo unagharimiwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Sambamba na barabara hiyo, Eng. Mwanga alisema mkandarasi wa barabara hiyo ataanza kujenga barabara nyingine ya km. 42.1 inayoanzaia Usa River hadi Kisongo kwa kiwango cha lami ambayo itakuwa na madaraja saba wakati ile ya Sakina hadi Tengeru ina madaraja makubwa mawili.

Naye mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari alisems uhaba wa ardhi bado ni tatizo kubwa kwenye wilaya hiyo kiasi kwamba hawana hata eneo la kujenga shule au zahanati.

“Maeneo yote yameuzwa na wenyeviti wa vijiji na madiwani, hivi sasa ukitaka kujenga shule au zahanati hakuna eneo hata moja. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utusaidie kufuatilia suala hilo licha ya kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi alishakuja na kuelezwa hali halisi ilivyo,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MEI 4, 2017.

No comments:

Post a Comment

Pages