HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2017

AFC LEOPARDS, TUSKER WAJIFUA VILIVYO KUJIANDAA NA SPORTPESA SUPER CUP KESHO

Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini, ambapo fungua dimba itakuwa ni kati ya Singida Utd na AFC Leopards, mechi ya pili itakuwa ni kati ya wenyeji Yanga na Tusker Fc na Juni 6 mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Simba vs Nakuru Nakuru All Stars na mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Gor Mahia Vs Jang'ombe Boys Fc. Picha kwa hisani ya Montage Ltd.
MAZOEZI YA TUSKER.
Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, jana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya 'SportPesa Super Cup', inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru. Mshindi wa michuano hiyo atapambana na timu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya England, nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Pages