HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 02, 2017

MAZISHI YA NDESAMBURO KUFANYIKA KWA SIKU MBILI MFULULIZO

Kikao cha Wanafamilia,Viongozi wa siasa na Viongozi wa Dini kikifanyika nyumbani kwa marehemu Ndesamburo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yake.
Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini

MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki katika mazishi hayo.

Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu. 

Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.

“Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.

Kutakuwa na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi huu tutakuwa na state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya kumbukizi ya maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema Golugwa.

Kwa upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto mkubwa wa marehemu Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali vinaendelea kwa ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa na maandamano.

“Kama unavyoonabado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona namna gani tunaweza kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa Moshi na taifa kwa ujumla “alisema Sindato.

Alisema wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na wafanyabiashara watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .

Mapema jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu  Ndesamburo  ikiongozwa na mtoto wake wa  Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.

Wakati kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya alikuwa akihudhuria vikao vya  Bunge la 11 ,vikao vya  Bajeti  ambapo alipata nafasi ya kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea taarifa rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.



Majira ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi la kuomba kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli baba yao amelala mauti.



Michuzi Blog ililifika KDC nyumbani kwa marehemu Ndesamburo na kushuhudia maandalizi ya shughuli za maziko yakiendelea huku waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya pembe ya nchi wakifika kutoa pole kwa familia ya marehemu.



Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.



Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani  Karatu mkoani Arusha.



Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Pages