HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2017

MAZISHI YA MAMA WA MTEMVU KATIKA PICHA


Enzi ya uhai wa Sitti Mtemvu
Mtoto wa Marehemu Amina Mtemvu (katikati) akisaidiwa na mama mtemvu kushoto na kulia Hellen Mwilima baada ya kuutambua mwili wakati walipofika katika Hospitali ya Lugalo kuuchukuwa mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiingizwa katika gari maalumu ukitokea Hospitali ya Lugalo kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi.
Mwili wa Marehemu Sitti Mtemvu ukishushwa nyumbani.
Wajukuu wa Marehemu Sitti Mtemvu wakiwa wamebeba picha ya marehemu.
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiwasili nyumbani ukipokelewa na waombolezaji ukitokea Hospitali ya Lugalo ukiingizwa ndani kabla ya kutowa heshima za mwisho.
Mchungaji Huduma Neno lililopo Mbagala Mgeninani, Yohana Msumule akiongosa kwa Ibada fupi baada ya mwili kuwasili nyumbani.
Familia ikiwa katika huzuni.
Wadogo wa Mtemvu na Mh, Mtemvu wakiwa katika majonzi
Mdogo wa Marehem Hamisi Mtemvu akitowa heshima za mwisho kabla ya kwenda makaburini.
Mdogo wa Marehem Hamisi Mtemvu akizungumza jambo na ndugu na familia yake baada ya yeye kutowa heshima za mwisho.
Sitti Mtemvu (kushoto) akizungumza na mama yake mama Mtemvu.
Abass Mtevu (kushoto) akizungumza na waaombolezaji.
Waombolezaji wakiwa wameubeba Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu mara baada ya kukiwazili katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mbunge wa Jibo la Temeke Mh, Abbas Mtemvu akitowa heshima za mwisho akiweka udongo katika kaburi la mama yake Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi mstaafu Tanzania, Davis Mwamunyange, (kulia) akimpa pole aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu.
Malima akiweka shada la maua na mkewe katika kaburi la mama wa Mtemvu.

Na Khamisi Mussa

Sitti Mtemvu ambaye alikuwa Mama wa aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alizikwa Juni 2, 2017 katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo Bi, Sitti Mtemvu alipata Elimu ya yake ya msingi katika Shule ya Jamiatul Islamiya iliyopo Mtaa wa Lumumba na Aggrey wakati huo ukiitwa New street na Stanley street.

Marehemu, Sitti alifunga ndoa na Hayati Zuberi Mtemvu 
mnamo miaka ya mwanzoni ya 1950, kipindi ambacho wote walijihusisha na shughuli za kisiasa za kudai Uhuru wa Tanganyika, 

Wakati mumewe alikuwa Katibu wa kwanza wa Chama Cha TANU chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, ambapo marehemu Sitti alijishughulisha na kuwahudumia wanasiasa hao wakati wapo kwenye mikutano ya siri iliyokuwa inafanyika nyumbani kwao

Kipindi hicho harakati za ukombozi zilikuwa zinafanywa kwa siri majumbani, ambapo nyumba ya  baba yake Marehemu Sitti iliyokuwa wanaishi ilitumika sana. Harakati hizo ziliwashirikisha wakinamama, Maria 

Nyerere, Sofia Kawawa, Bi Titi Mohamed na wengine, Marehemu pia alijiunga na vijana wengine kwenye mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika huko Arnatoglo Hall ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa vijana wasomi waliojipanga kutawala Nchi yao.

Hapo ndipo chimbuko la Chama cha TAA na hatimaye TANU ilipoanzishwa , vilevile alijiunga na Elimu ya  watu wazima na kusoma Lugha ya Kiingereza. Mnamo miaka hiyo marehemu alisafiri mikoa  mbalimbali kuanza harakati za kudai uhuru dhidi mkoloni,

Marehemu aliwahi kuwa kiongozi wa ngazi  mbalimbali katika umoja wa wanawake wa Tanganyika wakati huo na hata na baada ya  Muungano wa Tanzania. marehemu alifanya kazi Tanzania Cigarette Company mnamo miaka ya 1965 na 1973 wakati huo BAT na Bank of Tanzania na kustaafu mwaka 1973.

Baada ya kustaafu marehemu alijishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku mnamo mwaka 1987 marehemu alihamia nchini Ivory Coast Abidjan na kufanya biashara ya kuendesha mgahawa  wa chakula kwa kushirikiana na familia yake.

Marehemu alilazimika kurudi nchni baada ya machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo mnamo mwaka 1990.Marehemu alifariki mnamo Mei 30, 2017usiku kwa maradhi yaliyosababishwa na tatizo la sukarina umuri mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages