HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2017

Rais Magufuli Atoa Zawadi ya Idd El Fitri Yenye Thamani ya Mil. 10.9

KAMISHNA Msaidizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga, akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya Idd El Fitri kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli kwaVituo vya Yatima na Makundi Maalumu katika Maabusu ya Watoto Dar es Salaam, leo. (Picha na Frank Shija).
KAMISHNA Panga, akikabidi zawadi kwa Ofisa Ustawi  wa Jamii Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Yatima Kurasini, Dar es Salaam, Beatrice Mgumiro.
 KAMISHNA Panga, akikabidhi zawadi wa Sister Stella Selugenge wa Makao ya Yatima Msimbazi, Dar es Salaam.

Na Lilian Lundo, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El Fitri zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Panga amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.

“Mhe. Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.

Aidha, amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.

Vile vile, amevitaja vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma, Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.

Vituo vingine ni Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.

Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

Utoaji wa zawadi hizo ni utaratibu wa Waheshimiwa Marais tangu awamu nne zilizopita ambapo wamekuuwa wakiwapatia makundi hayo maalum zawadi za vyakula katika sikukuu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages