HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 11, 2017

Wakulima wa tumbaku kufaidika na ujenzi wa kiwanda kipya

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour, akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa Kiwanda cha Philip Morris Tanzania Mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo. Ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni.

Morogoro, Tanzania

Wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini wanatarajiwa kunufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni ya Philip Morris Tanzania Limited kuwekeza zaidi ya 60bn/- kwenye ujenzi wa kiwanda kipya ambacho kinajengwa kwenye maeneo ya Kingolwira ambao hipo katika Halmashauri ya Morogoro vijijini.

Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaidi wa tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia 34, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda.

Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa.

‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya viwanda. Lakini pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.

Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni wa kupongezwa, aliongeza Amour.

Nawapa changamoto wakulima wetu wa tumbaku kuongeza bidii ya kulima zao hilo kwani mnunuzi mkubwa wa zao lao kwa sasa ameamua kuja na kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Hii ni faida kwa upande wao. Aliongeza Amour huku akitoa rai kwa wafanyikazi ambao watapata ajira kwenye kiwanda hicho cha Philip Morris Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwani kutakuwa ni chachu ya kuvuta wawekezaji zaidi.’Uwekezaji kama huu ni taji kwa wasomi wetu kwani kunapanua ajira hapa nchini lakini nawaomba Watanzania ambao watapata hiyo fursa kuheshimu kanuni za ajira na kuwa na uhusiano mwema na wawekezaji kwani kiwanda kikifanya kazi zake kwa faida wafanyakazi pia nao watanufaika, alisema Amour.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano Philip Morris Tanzania Evans Mlelwa amesema uamuzi wa kampuni yake kuamua kujenga kiwanda hapa nchini kunatokana na mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, kiwango cha ukuaji wa uchumi pamoja na sera nzuri ya viwanda hapa nchini Tanzania.

‘Manufaa ya kiwanda hiki ni katika kuongeza mapato yatokanayo na na kodi kwa serikali, kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na pia kuongeza kwa ulimaji wa zao la tumbaku na kutoa ajira katika nyanja mbali mbali kama uzalishaji na usambazaji, alisema Mlelwa huku akiongeza kuwa kampuni yake itajikita zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu na kuhahakisha Wananchi wanaozunguka kiwanda wanapata maji salama kwa matumizi ya nyumbani.

‘Wanawake wamekuwa wakisahaulika sana. Sisi tuna mpango mzuri wa kuwawezesha na kuwainua kichumi na ndio maana nasema kiwanda kiwanda hiki kitakapokamililika kitakuwa na manufaa mengi kwa Wananchi wetu, alisema Mlelwa.

No comments:

Post a Comment

Pages